Wednesday, June 30, 2010

JUA LA SUMMER INAVYOWACHANGANYA WAZUNGU...


Hata Mbwa nao wanafurahia weather ya sasa apa Ulaya...
Huyu nae alikuwa amelewa mchana kweupeee na jua lote duuh...

Nami sikujivunga bwana alaaah...

Huyo kibonge nilimshuhudia akitoka kwenye mgahawa kupiga Baga zake 2 saafiiii alafu akamchukua shoga yake then haoooo...

Wengine wanatamani kukaa uchi kabsaaa ila basi 2...

HUYU NAE ABOMOLEWA NYUMBA...

Mkazi wa Kibaha akilia kwa uchungu jana baada ya kubomolewa nyumba yake na Tingatina kupisha upanuzi wa barabara! Sasa mimi nauliza aende wapii huyu mamaa jamaniii, au kuna hatua yoyote imeshachukuliwa mpaka sasa...

PARAGUAY YAWEKA HISTORIA LEO...


Hatimaye timu ya taifa ya PARAGUAY imeingia kwenye hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza katika Historia yao baaya ya kuitoa JAPAN kwa Penalti 5-3, ila ina mtihani mzito pale itakapokwaana na HISPANIA kwenye hatua iyo ya robo fainali kuingia nusu Fainali ya Kombe la Dunia.

HATIMATE SUGU NAE AGOMBEA UBUNGE KULE KWAO MBEYA MJINI...


Hatimaye mkongwe wa muziki wa kufokafoka 'aka' Bongo flava nchini MR 2 'AKA' SUGU, ametangaza kugombea ubunge kwenye jimbo la kwao kule Mbeya Mjini kwa tiketi ya CHADEMA! sasa nawauliza wadau kwa hatua aliyochukua Mr 2 mnaona ni sahihi kwasasa au amekurupuka?...

HATIMAYE WALE MARUBANI 2 WA AJALI YA NDEGE WAFARIKI DUNIA...


Hatimaye wale marubani 2 waliokuwa katika ndege ndogo iliyopata ajali leo katikati ya barabara ya kwenda Tanga wamefariki baada ya kujeruhiwa vibaya na hatimaye kupelekwa kutibiwa kwa dharula katika Hospital ya Magunga na hatimaye kuaga Dunia! Ndege hiyo ilitua ghafla barabarani baada ya kupata Hitlafu ya ghafla ilipokuwa angani na hatimaye kugonga gari ya watalii wa kiholanzi waliokuwa kwenye gari hilo, na hivi sasa maiti zimeshahifadhiwa katika Hospital ya Lugalo jijini Dar

Tuesday, June 29, 2010

MWANAMUZIKI SHAKIRA AKIMWAGA 'UNO' UKO KWA MANDELA JUZI...


Mwimbaji mwenye mvuto Duniani SHAKIRA, juzi alitumia muda wake mwingi kuwafundisha watoto wa kitongoji maarufu nchini Africa ya Kusini kiitwacho SOWETO jinsi ya kuucheza vizuri wimbo wake maalum wa Kombe la Dunia na alisema kauli mbiu yake katika Kombe hilo mwaka huu ni 'elimu kwa wote', palikuwa hapatoshi siku hiyo lol...

MAMBO YA MARADONA HAYO ALIPOKUWA ANACHEZEA NAPOLI YA ITALIA...

DUUH SIKIA HIYOO MUPYAA...

Golikipa wa timu ya taifa ya Ujerumani MANUEL NEUER leo kwenye mahojiano na Television moja ya Ujerumani amekiri kumdanganya refu ili asilikubali goli la jana la England kwa kugeuka haraka kuukamata mpira baada ya kudunda kutoka kwenye mlingoto wa goli 'aka' mwamba 'aka' mtambaa panya na kusema hayo mambo yapo kwenye michezo yoote duniani kutegemea na hali ilivyo kwenye mchezo duuh! Je ingekuwa kipa wa kiBongo angekubali kwamba kafanya udanganyifu ili aisaidie timu yake? si angebisha mpaka Yesu arudi...

CAMERA YANGU MTAANI...

Sikuzote unaambiwa we baba mpende mwanao na uwe na muda na mtoto alaah, usilete mambo yale ya kikoloni kilakitu umwachie mkeo, mbona wakati mnamtafuta uyo mtoto mlikuwa wote?...
Wanenguaji mahiri wa FM ACADEMIA Lolei, Titi na Fatma wakiwa Back stage wakijitayarisha kuingia Stejini...

Rapa mahiri wa FM ACADEMIA TOTOO KALALA akila pouzz na mashabiki wake juzi kwenye onyesho lao...

Mnenguaji mkongwe nchini LILIAN INTERNET wa bendi ya TWANGA PEPETA akinengua jukwaani juzi. Kwa wale wapenzi wa Dansi watamkumbuka sana tangu alipovuma na bendi ya DIAMOND SOUND 'wana ikibinda nkoi' enzi zao pale New Silent Inn MWENGE kwa papaa Rwegasira, alikuwa tishio sna na hata sasa wanenguaji wa kike chipukizi bado wanamgwaya kwa sana 2 ila naskia tayari ni mjamzito! Kama ni kweli sie kama Kinyaiya's blog tunamtakia kheri kama mama mtarajiwa...

Sunday, June 27, 2010

JAMANI ETI CAPELLO AJIUZULU AU WANAMUONEA?...

Baada ya kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Germany, kuna mjadala unaendelea hapa Uwingereza kwamba eti kocha wa England Mr FABIO CAPELLO ajiuzulu au aendelee? sasa wadau wa soka na mashabiki wa hapa wameganyika na kuchanganyikiwa kwa kipigo icho kilichoitoa timu yao mashindanoni, sasa kama wewe ni shabiki wa soka unaejua mwenendo mzima wa timu ya England unaona ni sahihi kwa Capello kujiuzulu au wanamuonea 2 buree?...

Wachezaji wa ENGLAND wakiwa hawaamini macho yao kwa kipigo kitakatifu walichokipata kutoka kwa Ujerumani ingawa eti wanasema kwamba eti kukataliwa bao lao alilofunga Lampard ndio limewafanya wachanganyikiwe na kupelekea kufungwa hayo mabao mengine, wakati nionavyo mimi kama Ben ni kwamba Germany walikuwa wazuri zaidi kwa kilaki2 Uwanjani kuliko England, au mnasemaje wadau...

WAGHANA NA WAAFRICA WALIVYOSHEHEREKEA USHINDI JANA APA LONDON...

Yaani kilaki2 kiliwekwa Rangi au Bendera ya GHANA jana, Hongera kwa waghana na AFRICA NZIMA KWA UJUMLA...
Kila mwafrica alisheherekea kwa jinsi anavyojua bila kuvunja sheria


Ilikuwa ni patashika baada ya filimbi ya mwisho kushiria GHANA wameingia robo fainali na kuweka Historia tangu ilivyofanya Cameroon kwa mara ya mwisho...


YALIYOJIRI KWENYE SHINDANO LA REDDS MISS ILALA JANA NDANI YA UBUNGO PLAZA...

Mrembo BAHATI CHANDE 'katikati', ndie aliyeibuka kidedeo na kuwapiku warembo wote katika shindano la kumtafuta REDDS MISS ILALA lililofanyika jana ndani ya ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar.
Mrembo anayemaliza muda wake SLYVIA SHALLI 'kushoto' akimvisha Taji la Redds Miss Ilala mrembo mpya BAHATI CHANDE...


Kama kawa wazee wa Ngwasuma FM ACADEMIA walikuwepo kuto burudani na hapa pichani wanenguaji wake wakimwaga 'mauno' yaliyowapagisha wa2 ukumbini...


Waimbaji wa bendi ya FMA ACADEMIA 'wazee wa ngwasuma' walitoa burudani ya kufa m2 jana katika ukumbi wa Ubungo Plaza...
Majaji wa shindano ilo la mic Ilala wakiongozwa na Uncle LUNDENGA 'kushoto', wakisubiri kutangazwa mshindi ambaye aliibuka mrembo BAHATI CHANDE...

Mamic wakifanya shoo ya ufunguzi jana iliyowavutia sana watu waliofika jana ndani ya ukumbi wa Ubungo Plaza...


Burudani ya SARAKASI ilishika kasi yake na kuwa kivutio pia...









MSIONE KIMYA WADAU NILIKUWA SAFARINI KURUDI LONDON JANA...

Hapa ni baada ya kuoga na kupumzika ndipo nikaamua kutoka nje kupeleka zawadi za watu mitaa ya kati maana wabongo wakisikia m2 anaondoka kwa kutuma haooo...

Hapa ni baada ya kufika LONDON, naelekea kwangu kupumzika kutokana na uchovu

Hapa nimeshaingia LONDON na nimeingia Underground kuchukua Train ili nielekee home fasta maana nimechoka sanaaa...
Hapa ni HEATHROW Airport mjini London na ndio nimetoka kuchukua Begi langu kubwa tayari kwa safari ya kuelekea home...





Kwa hakika safari ilikuwa ndefu yenye uchovu mwingi jana maana si munajua ukipanda EMIRATE lazma wakushushe kwao DUBAI alafu ndio uunganishe pipa lingine looh...



Hapa nilipofika DUBAI nikaamua kuperuzi kwenye Laptop yangu ili niwawekee japo picha chache za safaRi yangu ya kurudi tena LONDON jana...




Hapa ni uwanja wa ndege wa Dubai na kama kawaida yake pilika mzake ni nyingi kutokana na wageni mbalimbali na abiria wa mashirika mbalimbali ya ndege yanayopitia hapa!
Na wakati nikiwa hapa jana usiku nilijaribu kupita ktika maduka mbalimbali kuangalia vi2 na hatimaye nikaingia kwenye duka la saa na kukuta saa mbalimbali za thamani kama unazoziona hapo juu aina ya RADO na kuna saa moja niliipenda ila nilivyouliza bei yake nikaambiwa ni Dola 2920, kisa ina madini ya Diamond ndani yake looh...


Nikiwa uwanja wa ndege wa DUBAI nikisubiri kuonganisha ndege kurudi LONDON jana usiku...






Wednesday, June 23, 2010

CAMERA YANGU MTAANI...


Hapa niliwabamba rafiki zangu kuanzia kushoto ni mpiga Tumba maarufu wa bendi ya Twanga Pepeta MCD, akifuatiwa na mshambuliaji hatari wa timu ya SIMBA na Taifa starz MUSA HASSAN 'MGOSI', totozz n mie mwenyewe...

Nikiwa na wadogo zangu akiwemo chipukizi wa Bongo Flava anaekuja juu DIAMOND, kulia kwangu.

Nikiwa na wanenguaji wa Twanga Pepeta kina AISHA MADINDA na wenzake walipokuja kunitembelea KINYAIYA'S PUB iliyoko nyuma ya Mango Garden Kinondon jana...

Hapa nilimfuma mwimbaji hodari wa Twanga Pepeta aitwae CHALZ BABA akifanya mpango wa kuapata japo Chips Vumbi ili apoze REJETA YAKE...

Watotozzzz...

Kama kawa Camera yangu iliwabamba pia kutoka kushoto ni KALALA JUNIOR wa Twanga Pepeta, MCD pia wa Twanga na Mshambuliaji wa Simba na Taifa Starz MUSA HASSAN MGOSI...

Niliwahi kusikia kwa watu wakisema eti PAKA huwa wanapendaga Starehe sana ila sasa nimeamini, maana jana nilimtembelea rafiki yangu kwakwe nikakuta kumbe anafuga Paka wake 2 anaowapenda sana, na cha ajabu niliwakuta Paka hao wakiwa wamelala kwenye Makochi kwa Staili tofauti kama wanavyoonekana hapa, mmoja kalala kama mtu kwenye Kochi kubwa na mwingine kalala na mdoli wake apo kulia kwenye Kochi dogo! Na mpaka tunamaliza maongezi yetu na mie kuaga bado hakuna hata Paka mmoja aliestuka usingizini duuh, hii imekaaje wadau...

Mchec Paka huyu alivyoukumbatia mdoli huku akiuchapa usingizi looh...

Chec huyu mwingine alivyolala kama mtu bila wasiwasi...

Monday, June 21, 2010

DIAMOND MUSICA WALIVYOPAGAWISHA WATU JANA USIKU...


Kiongozi wa bendi ya DIAMOND MUSICA ya jijini Dar MULE ZIRI akiwaongoza waimbaji wake kufanya Shoobiz ya kufa m2 jana ndani ya Ukumbi wa MANGO GARDEN. Huyu jamaa mwanzo alikuwa katika Bendi ya FM ACADEMIA 'wazee wa ngwasuma' kabla ya kupewa dau kubwa na kuhamia Diamond Musica, nadhani wapenzi wa muziki wa Dansi nchini mtakuwa mnamfahamu vizuru huyu bwana kutokana na uhodari wake wa kucheza jukwaani...

Kwa hakika wanenguaji wake walipagawisha sana jana...

Hata 'WATHUNGU' nao walichengua na sebene la Bendi hiyo na kujikuta wakiiacha viti vyao duuuh...

Kwa hakika watu wali enjoy sana kwenye Onyesho hilo na hii picha inaonyesha dhahiri jinsi watu walivyopagawa...
Website counter