Wednesday, June 23, 2010


Watotozzzz...

Kama kawa Camera yangu iliwabamba pia kutoka kushoto ni KALALA JUNIOR wa Twanga Pepeta, MCD pia wa Twanga na Mshambuliaji wa Simba na Taifa Starz MUSA HASSAN MGOSI...

Niliwahi kusikia kwa watu wakisema eti PAKA huwa wanapendaga Starehe sana ila sasa nimeamini, maana jana nilimtembelea rafiki yangu kwakwe nikakuta kumbe anafuga Paka wake 2 anaowapenda sana, na cha ajabu niliwakuta Paka hao wakiwa wamelala kwenye Makochi kwa Staili tofauti kama wanavyoonekana hapa, mmoja kalala kama mtu kwenye Kochi kubwa na mwingine kalala na mdoli wake apo kulia kwenye Kochi dogo! Na mpaka tunamaliza maongezi yetu na mie kuaga bado hakuna hata Paka mmoja aliestuka usingizini duuh, hii imekaaje wadau...

Mchec Paka huyu alivyoukumbatia mdoli huku akiuchapa usingizi looh...

Chec huyu mwingine alivyolala kama mtu bila wasiwasi...

No comments:

Website counter