Monday, October 4, 2010

WAGENI WANGU WALIOKUWEPO KWENYE KIPINDI CHANGU CHA JUZI JUMAMOSI TBC1...


Katika kipindi changu cha juzi Jumamosi nilikuwa na swahiba wangu MAIMARTHA ambaye amerudi tena baada ya mapumziko ya msiba wa Mchumba wake PERFECT KAGISSA aka P'DIDDY, na show ilikuwa nzuri sana kama kawa kwa wale walioangalia na makamuzi yalikuwa ya Hatwaariii...

Mgeni wangu wa kwanza kwenye kipindi changu cha juzi alikuwa ni mcheza Fillamu hodari nchini aitwae HISANI MUYA aka 'TINO' ambaye tulizungumza mengi na alijibu maswali ya watazamaji na kikubwa zaidi alichozungumzia ni kuhusu yeye kuandaa Filamu ya kwanza nchini inayohusiana na mambo ya 'USHOGA' na athari zake kwa jamii na alisema yeye ataigiza kama 'SHOGA' mkuu katika filamu hiyo ili kufikisha ujumbe kwa Jamii duuh, ebu tusubiri kuona itakavyokuwa na kama una swali lolote kumuhusu yeye basi waweza kuniandikia maswali myako nami nitamuuliza ili aweze kuwajibu....
Mgeni wangu wa pili kwenye kipindi changu juzi alikuwa ni mshambuliaji Hatari wa timu ya SIMBA na timu ya Taifa ' TAIFA STARZ' aitwae MUSSA HASSAN 'MGOSI' ambaye tulizungumza mengi kuhusiana na soka na kama una maswali kwake waweza niandikia nami nikamuuliza moja kwa moja ili aweze kuwajibu apa Bloguni...








1 comment:

Johprise said...

Ben napenda sana kipindi chako na mai, shortly nawapa big up sana coz u know what u r doing and what your fans need. Pia nimefurahishwa sana na ujio wa Hassan Muya kwenye show, i really like him coz he is the same serious as u do and anafanya kweli kwenye movie industry. i cant wait to see that new movie of his.

Website counter