Sunday, October 30, 2011

HARUSI YA MWIGIZAJI SKINER ALL ILIVYOFANA...


Wiki iliyopita Mwigizaji chipukizi wa Filamu nchini SKINER ALLY alifunga ndoa katika sherehe iliyofana na kufuatiwa na 'Mnuso' wa nguvu nyumbani kwao Bi, harusi maeneo ya Magomeni jijini Dar na kuhudhuriwa na Mastaa mbalimbali wa Filamu nchini...

Mwanamuziki MAUNDA ZORO nae alikuwepo kwenye 'MNUSO' huo...

Funz kibao nilikutana nao Mnusoni...

Mimi, SKINER na mumewe, tukiwa kwenye pouzzz...

Mwigizaji mkongwe wa Filamu nchini Bi. JOAHARI nae alikuwepo bega kwa bega kumpa TAFU bi Harusi HAZRA aka SKINER...

Mwigizaji IRENE UWOYA yeye alikuwepo kuongoza msafara wa kumtoa ndani Bi. harusi...

Nilipata Fursa ya kupiga picha na Mashabiki wangu wengi walionisalimia...

Mshikemshike wakati wa Maharusi kutoka nje kuelekea HONEYMOON...

Yaani BIRIANI ya siku hiyo ilikuwa BALAA kwa utamu wake daaah...

Friday, October 14, 2011

SAFARI YANGU YA KURUDI 'BONGO' ILIVYOKUWA JUZI JUMANNE...


Juzi Jumanne usiku nilisafiri tena kurudi BONGO nikitokea London UK. kwa ujumla safari yangu ilikuwa poa sanaa na nilifika Dar kesho yake mchana bila kokoro yoyote...

Heathrow Airport London naelekea kwenye Gate langu...

Na hapa sasa ni wakati nikiwa nje ya Nyumbani kwangu pale London nikijitayarisha kuelekea Airport...

Nikiwa na mdogo wangu AYSHA ndani ya Heathrow Airport London...

Ndani ya 'PIPA' kama kawa kuitafuta Bongo kudaadekiii...

Sasa kwa Bahati nzuri Ndege yetu ilipitia juu ya kilele cha Mlima 'KILIMANJARO' na sie abiria tukauona vizuri pale kwenye 'shimo' juu ya Kilele chake! Ilikuwa raha sanaaa na wengi walifurahia kuona kilele cha Mlima huo mrefu kuliko yooote barani Africa...


Na mwisho kabisa ndani ya Ndege juzi nikakutana na rafiki yangu kwa mara ya Pili, naye si mwingine ila ni Kiungo nyota wa timu ya taifa ya GHANA na klabu ya INTER MILAN ya Italia SULLEY MUNTARI, ambaye ingawa alikuwa amelewa kwa Masanga bado alikuwa mchangamfu kwenye maongezi yetu usiku mzima tuliokuwa tunasafiri kwenye ndege yetu na aliniambia anaelekea Nairobi nchini Kenya ila atafanya juuu chini kutafuta nafasi ya kuja kunitembelea Tanzania maana anaisikia tu ingawa hajawahi kufika...

WEEKEND ILIYOPITA 'NILIPOALIKWA' NA RAFIKI ZANGU WA NORTHAMPTON...
Weekend iliyopita nilialikwa kwenye Part na rafiki zangu waishio mji wa NOTRHAMPTON ambao upo umbali wa kama masaa 2 kwa gari kutoka apa London UK. kwakweli nimeufurahia ukarimu wao waluionionyesha kwani wengi wao walikuwa wananisikia tu kwa jina lakini hatukuwahi kuonana 'LIVE' so ilikuwa ni furaha kwa wote kukutana, na walikuwepo watu wa aina mbalimbali kwenye Part hiyo kwa ajili ya chakula na kinywaji na kila mtu alijishebedua atakavyo!

Marafiki walikuja wengi sana kujumuika nasi sikuhiyo...


Wakuu wa 'KIKOSI' tukishow Love...


Kuanzia kulia ni IBRA, MIMI, ESTHER na MPEMBA...

Kuanzia kulia ni DIDA FACION, LILLA, MIMI, MPEMBA na ESTHER...

Baada ya 'VURUGU' zangu kuisha nikakusanya vyangu na kuanza 'mdogo mdogo' kurudi Kitaani kwangu LONDON bila kokoro atiii...

KUTHAMINIWA KWA WANYAMA ILIVYO 'TOFAUTI' KATI YA ULAYA NA AFRICA...


Kule kwetu barani Africa wanyama kama MBWA, PAKA na wengineo huwaq hawana 'THAMANI' kabsaaa wala haki ya kupata matunzo au huduma za Afya zinazostahili labda kwa watu wachache na tena ni wale wa sehemu za 'UZUNGUNI' ingawa mie Binafsi nawapenda Wanyama hawa na ninawafuga kule Home kwangu Kinondoni jijini Dar! Wakati Barani Ulaya wanyama hawa huwa wanathamini wa na kuheshimika mpaka kupandishwa kwenye Mabasi na Matrain kokote pale, hali ni tofauti na kule kwetu Africa ambapo wanyama hawa wanatumiwa zaidi Kishirikina na hata maranyingi kuteswa kama picha hii inavyoonesha hapo juu bila sababu za Msingi. Sasa kitendo kama hicho cha kumuweka mnyama 'MSALABANI' kawa hao mabwana walivyofanya kwenye picha wangekifanya hapa Ulaya, wangefungwa miaka mingi Gerezani na Faini juu...


Sasa hali ya kuthaminiwa kwa wanyama huku barani Ulaya ni tofauti na kwetu Africa, kiasi kwamba kwamba kwa huku Ulaya Mnyama anawekewa mpaka Bima ya Maisha na huwa wanapatiwa matibabu ya hali ya juu kuliko hata Binadamu wa kawaida na huwa waachiwaga 'URITHI' wa majumba na Pesa za kuwatunza...

Mie huwa nabaki kuwaangaliaga tu ila natafakari sikumoja na mimi niingie na MBWA kwenye Daladala nikirudi Bongo alafu nione 'MTITI' wake utakavyokuwa haaa haaaa...

Tuesday, October 4, 2011

http://youtu.be/YKv90WGMtGI

FANYA HAYA 'KUNOGESHA' NDOA YAKO....


WAPENZI wasomaji wangu, naomba leo niende moja kwa moja kwenye mada yangu ya wiki hii ambayo kwa kiasi kikubwa inawagusa wanawake. Nazungumzia mambo ambayo mwanamke anatakiwa kuyazingatia ili aweze kumshika ipasavyo mumewe na kuinogesha ndoa yake.

Ni mengi anayostahili kufanya mke kwa mumewe lakini kwa leo nitazungumza machache ambayo naamini yatakuwa na manufaa kwako.

Timiza wajibu wako kama mke
Mwanamke anayemjali mume wake ndiye anayetimiza wajibu, lakini wengi hujikuta wakisalitiwa au kuachwa kabisa na waume zao kutokana na ufahamu mdogo ama dharau ya mambo madogo.

Ni busara kutambua kwamba, ndoa haina mambo madogo. Kila kitu kina umuhimu mkubwa kulingana na nafasi yake sambamba na utekelezaji wako. Mfano, kumpokea bahasha anaporejea kutoka kazini ni kitu kidogo tu ambacho wewe unaweza kukidharau lakini thamani yake kwa mumeo ni kubwa kuliko unavyofikiria.

Tambua kuwa, mwanaume harogwi kwa limbwata la sangoma, mahaba peke yake yanatosha kumshika vilivyo. ‘Ukimhendo’ kwa kiwango kitakachomridhisha, hatawaza kukuacha. Unawezaje? Jibu ni rahisi, muoneshe unampenda na uthibitishe mapenzi yako kwa vitendo na si kwa maneno tu.

Daima hili liwe kwenye akilini yako, mwanamke kupitia mapenzi yake ana uwezo mkubwa mno, lakini lazima awe anajua kutimiza wajibu wake kwenye maisha ya ndoa.

Kama mumeo anakuacha, ujue kuwa kuna mambo unayomkosea na kuyafanya mapenzi yako yageuke kuwa kero kwake. Unyenyekevu kwa wanawake wa kisasa kimekuwa ni kitu adimu sana kiasi ambacho kimekuwa kikihatarisha ndoa zao.

Wanaume wanawapenda wanawake ambao hujionesha waziwazi kuwa wenyewe ni wasaidizi wao wakuu katika masuala mbalimbali. Hawavutiwi na wale ambao hupuuza mambo kwa visingizio visivyokuwa na maana.

Kuwa mjanja kiana
Sababu ya wanaume kuwapenda wanawake wajanja ni kukwepa aibu wanazoweza kuzipata pindi watakapokuwa kwenye uhusiano na wanawake washamba.
Huogopa kujiingiza katika mapenzi na watu wasio na uelewa mpana wa mambo ambao huwafanya kuwa mafundi wa kuiga mambo yasiyofaa.

Washamba mara nyingi huwa ni malimbukeni, hujifunza mambo yasiyokuwa na faida kwa imani kwamba naye ataonekana mtu kati ya watu. Wanawake wa aina hii ni rahisi kuwaingiza wenzi wao katika hasara kubwa. Hawakawii kusaliti pamoja na kudanganyika kwa mambo madogo. Wanawake malimbukeni huharibika vibarazani na saluni kutokana na sifa kubwa ya umbeya kwenye sehemu hizo. Wanaume wasiokuwa na subira hujikuta wakiwaacha wake zao mapema, mara tu wanapoanza kuhisi nyendo zisizoeleweka kwa wenzi wao. Tumekuwa tukishuhudia wanawake malimbukeni wakiiga tabia za ulevi wa pombe, kuwa na makuu katika maisha yao kutokana na kuwaona wenzao wakiwa hivyo. Hili ni tatizo ambalo wewe mke wa mtu unatakiwa kuliepuka ili uishi milele na mumeo. Siku zote mwanamke mjanja hawezi kuiga hovyo hovyo, siku zote anajua kitu cha kuanzia na kinachofuata. Hadanganyiki kirahisi na hiyo ni sifa kubwa ambayo inaweza kuinogesha ndoa yako kwa kiasi kikubwa.

JANA NILIPOTEMBELEA 'SHOOPING CENTRE' KUBWA KULIKO 'ZOOOTE' DUNIANI APA LONDON...


Jana nilitembelea SHOOPING CENTRE kuubwa kuliko zooote Duniani ambayo ni mpyaaa kabsaaa kujengwa maeneo ya Stratfold apa London Uwingereza na inasemekana ina maduka zaidi ya elfu 30,600 daaah...

Mall hii ya Hatari imezungukwa na kila aina ya usafiri wa kuwezesha watu kufika kupata mahitaji, yaani kwa ujumla Miundombinu imetimia......

Kumbuka hii ndio SHOOPING CENTRE kubwa kuliko zoooote Duniani kwasasa, kwaiyo mpaka watalii kutoka nchi mbalimbali huja kutembelea kujionea ilivyojengwa na inasemekana Waingereza wametumia miaka 4 kukamilisha ujenzi wake duuuh...

Kuna njia nyingi za kuingilia na hii ni mojawapo kutegemea unatokea upande gani hasa...

Miundombinu kama kawa imetimia kwenye Mall hiyo na hapa mpaka 'Underground Train' pia ipo kama kawa kudaadeki...

Monday, October 3, 2011


Ndani ya hiyo Shooping Center kuna kila aina ya Migahawa yenye majina makubwa Duniani, yaani kwa hakika kwenye Mashindano ya Olympic ya mwakani apa LONDON mambo yatanoga saanaaa...

MWAMVITA na Mamaa SUE nilikuwa nao sambamba nilipoingia kwenye Mgahawa wa NANDOZ...

Mambo ya 'NANDOZ' sio mchezo banaa, nayo ipo humo humo ndani ya MALL...

Mie izi 'SPICE' za Nandoz huwa nazipendaga sanaaa...

Maduka ya kila aina na hakuna kitu ambacho utakitaka utakikosa...

Sunday, October 2, 2011

KUELEKEA JUMAPILI YA KESHO MAKANISANI...


AMANI iwe kwenu enyi waheshimiwa wasomaji wangu. Natumai nyote kwa ujumla wenu, mu wazima kiasi cha kuendelea na shughuli zenu salama ila leo nina mawili matatu, kwa ajili ya hawa wanaovaa mavazi yasiyofaa katika nyumba za ibada.

Jamani katika suala la mavazi ni vyema kufahamu kuwa, kila mahala kuna utaratibu wake wa mavazi wazungu wanauita ‘dress code’. Nguo ya ofisini si sawa na ile inayovaliwa msibani, au ile ya msibani si sawa na ile inayovaliwa kwenye sherehe. Mavazi ya mwalimu si sawa nay ale ya daktari n.k

Mambo haya hayaishii huko, kwani huendelea mpaka kwenye nyumba za ibada. Katika kipindi cha hivi karibuni kumezuka mitindo mipya ya kufanya nyumba za ibada kama sehemu ya kufanyia mashindano ya urembo hususani kwa wanawake.

Sikatai kuwa, kila mmoja wetu anatakiwa kuwa msafi mbele za mungu lakini usafi huu haumaniishi kuvaa suruali za kubana, kuacha baadhi ya maeneo nyeti ya mwili nje ama kuvaa nguo fupi!

Nafahamu kuwa nyote mnaelewa fika mavazi maalum ya kuvaa katika nyumba za ibada na badala yake mnafanya makusudi. Mimi nafikiri huu ni ulimbukeni na wala si vinginevyo.

Naelewa si wengi mnaofahamu athari za nyinyi kuvaa mavazi yasiyofaa hususani mnapoenda sehemu takatifu kama vile kwenye madhabahu ya mungu. Na laiti mngeelewa msingethubutu hata siku moja kuvaa mavazi hayo.Ninapoongelea madhabahu nafikiri kila mmoja wenu anafahamu kuwa ni dini gani hasa ninayoilenga.

Miongoni mwa athari hizo kwanza ni kuwajenga watoto waiokuwa na hofu juu ya muumba wao. Kwani watakuwa wakifuata namna mnavyofanya nyie mliowatangulia na hivyo kuvaa mavazi hayo yasiyofaa kanisani.

Na kwa kawaida ya watoto hawataishia hapo. Kwani kitendo cha kuingia na vimini kanisani vitawatia majaribuni waumini wakiume, jambo litakalosababisha matamanio juu yao. Kwa mantiki hiyo hakutakuwa na mawazo ya mungu tena, ispokuwa utawala wa shetani. Kitakachoendelea hapo hebu pata picha ………

Niseme ukweli kutoka moyoni kuwa, katika hili sina tatizo na waumini wa kike wa madhehebu yote ya dini ya kiislamu.Kwani wao wanaelewa fika namna ya kuvaa wakiwa katika sehemu zao za ibada. Wao hujisitiri hasa kama vitabu vya dini vinavyoamuru. Na kwa kuwa wao hawana utaratibu wa kuchanganyika wakati wa ibada, hili kwao bado sio tatizo sana.

Katika haya mavazi yasiyofaa, ningependa kuwageukia na nyie maharusi hasa wa kike. Ninachoelewa mimi ni kwamba, huwa mnapata mafunzo ya aina mbalimbali kwa muda uisopungua wik moja kabla ya ndoa. Darasa juu ya mavazi yanayofaa siku ya ndoa ni moja wapo ya mafunzo hayo.

Cha kushangaza siku ya ibada ya ndoa, mnakuja madhabauni mkiwa mabega wazi. Hivi huku ni kusahau au dharau?
Hebu muogopeni mungu wenu. Heshimuni nyumba za ibada. Pale sio sehemu ya kuonyeshana mavazi, ni sehemutu ya kukutana kifikra na mungu wako. Hivyo si vibaya ukajiandaa vyema kuingia katika mazingira hayo. Vaa yale yanayaokubalika kwa mungu wako na si vinginevyo.

Hili suala la kuwekewa ’ fashion police’ kwenye milango ya makanisa ni aibu kwa waumini na kanisa kwa ujumla. Kwani hainiingii akilini, eti mwenzenu badala ya kuingia kusali, akae mlangoni kukagua nani kavaa vazi gani?

Badilikeni! Muogopeni mungu wenu, vaeni kama ilivyoamriwa kwenye vitabu vyenu vya dini, Ikiwa mnahitaji mifano angaalieni wahudumu wa kanisa ama masista wanavyovaa, hilo ndilo jibu sahihi la mavazi yanayotakiwa kuvaliwa kwenye nyumba zenu za ibada.

Narudia tena BADILIKENI!

Friday, September 30, 2011

SIKIA MPINI WA 'NGWIJI' DIBLO DIBALA, MPIGA GITAA LA 'SOLO' NAMBA MOJA BARANI AFRICA...

HII NI RIPOTI MAALUM YA UKWELI NA TUNAOMBA HAYA MAMBO YASHUGHULIKIWE NA WAHUSIKA JAMANI...WIKI iliyopita mfungwa aliyemaliza kifungo chake alieleza kwa kina jinsi alivyoingiza simu na bangi gerezani na kuzitumia kama mradi wake wa kujipatia pesa. Pia watu wengine wawili waliowahi kufungwa katika magereza ya Segerea, Mwanga na Karanga mkoani Kilimanjaro nao wameeleza jinsi walivyokuwa wakitoa pesa kupewa chakula kizuri gerezani.

Biashara ya chakula
Mmoja wa watu hao alisema: “Ukitaka kupata chakula kizuri katika Gereza la Segerea ilikuwa lazima ununue kutoka kwa wapishi.

“Unachoweza kukifanya ni kuzungumza nao halafu unawalipa kwa wiki. Chakula ambacho unaweza kukipata ukiingia mkataba huo ni mboga iliyoungwa kwa mafuta na ugali”.

Anasema kama huna cha kuwapa kwa wiki hiyo unaweza kuwasiliana na ndugu yako akampa fedha mmoja wa askari magereza wanaopeleka mahabusu mahakamani akaziingiza magereza.

Mtu mwingine ambaye ameonja kifungo katika gereza la Karanga na Mwanga mkoani Kilimanjaro alisema; “Rushwa ndani ya magereza ni kubwa kiasi kwamba, ukiwa huna pesa ya kuhonga askari, mnyapara au daktari wa magereza, utakiona kifungo kibaya mno”.

Akisimulia jinsi alivyoingiza simu magereza, Mfungwa huyo ambaye alitumikia kifungo cha miaka minne katika magereza mkoani Kilimanjaro, alisema aliingiza simu gerezani baada ya kushuhudia askari mmoja wa magereza akimpiga mfungwa ambaye baadaye alifariki dunia.

Kutokana na tukio hilo, askari huyo baada ya kuambiwa na baadhi ya wafungwa kuwa aliyeshuhudia tukio hilo ana uwezo wa kuvujisha taarifa hiyo kwa watu wengine nje ya gereza aliamua kujenga naye urafiki.

Anasema askari hiyo alimwahidi kuwa atamsaidia kuingiza simu gerezani ambayo aliitumia muda wote kuwasiliana na mke wake na marafiki zake.

Alisema, "Simu hiyo ilinisaidia kupata habari za kila siku za familia yangu na pia niliwapigia watu mbalimbali bila matatizo,"

Mfungwa huyo, anasema uhalifu unaofanywa na askari magereza ndio unaosababisha kutoa mwanya kwa wafungwa wa kiume kujiingiza katika vitendo vya kuvunja sheria, ikiwamo kuingiza bangi, simu na kufanya mapenzi na wanawake wa nje ya gereza.

Anasema wakati mwingine askari magereza wanashirikiana na wafungwa kuiba mali za gereza, ikiwamo mahindi na mbolea na kuuza uraiani.

Anatoa mfano kuwa, kuna siku alishirikishwa na askari mmoja katika Gereza la Karanga kuiba magunia saba ya mahindi.Alifahamisha kuwa waliyapakia katika lori kwenda kupanda shamba la gereza, lakini badala yake waliyauza kwa watu waliokubaliana na askari huyo.

Alidai kuwa baada ya kuuza alipata mgawo wake pamoja na wafungwa wenzake wanne waliokuwamo ndani ya gari hilo.

Mbali ya kushirikishwa katika wizi huo wa mahindi ya magereza, pia alidai kuwa wahi kutumiwa na askari huyo kuiba mbolea ya ruzuku ambazo zinatolewa na serikali kwa gereza hilo.

Vilevile, kwa kushirikiana na baadhi ya askari magereza alisema aliwahi kuingiza vitu mbalimbali gerezani ikiwamo pesa na bangi kwa ajili ya kuiuza.


Kuhusu kufanya mapenzi na wanawake nje ya magereza, alisema hilo ni jambo linalowezekana kabisa. Anasema wafungwa wengi wenye uwezo huwapa pesa askari wasiokuwa na maadili hivyo kupangiwa kufanya kazi nje ya gereza.

Alisema: "Unachotakiwa kufanya ni kupanga na askari magereza ambaye anampa taarifa mke wako kuwa mtakuwa wapi."

Mfungwa huyo anasema: Akifika mke wako, askari magereza anakuruhusu kwenda sehemu yoyote ya kificho karibu na eneo hilo.Alifahamisha njia nyingine ambayo inaweza kukufanya ukutane na mke wako ni kwenda kulazwa hospitalini.

“Asilimia kubwa ya wafungwa wanaolazwa hospitali huwa sio wagonjwa, bali hupata kibali cha kwenda kutibiwa baada ya kutoa chochote kwa daktari wa gereza,” alifahamisha na kuongeza."Usione ndugu yangu wafungwa wengi wamelazwa hospitalini, wengine wanakuwa sio wagonjwa, wapo huko kupumzika na kupata nafasi ya kuonana na ndugu zao kirahisi,"

Alieleza kuwa: “Ukipata kibali cha kwenda kutibiwa hospitali, unaweza kumpa chochote askari anayekulinda akakuruhusu kukutana na mkeo usiku.

Vilevile, sehemu nyingine ambayo mfungwa anaweza kuitumia kukutana na mke wake ni pale anapopangiwa kufanya kazi kwenye mashamba ya maafisa wa magereza ambako hupata uhuru zaidi.

"Mfungwa kufanya kazi kwenye mashamba ya maafisa wa magereza ni kosa ndiyo maana wanapokuchukua huwa wanatoa uhuru kiasi, hasa kwa wafungwa wanaokaribia kumaliza vifungo, au wenye tabia njema," alifahamisha.

Hata hivyo alisema, ingawa kuna wafungwa ambao wapo hospitali kwa ajili ya kuishi vyema, wapo wafungwa ambao wanaumwa ambao wanahitaji kupatiwa matibabu, lakini hawapelekwi hospitalini.

Alidai kuwa kuna usanii mwingi katika magereza, kwani hata Tume ya Haki za Binadamu wanapopita kuangalia hali za wafungwa baadhi ya viongozi wa magereza hutandika mashuka mapya katika magodoro ya wafungwa, lakini wakiondoka tu huyaondoa haraka.

Ripoti ya Tume
Ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ya mwaka 2009/2010 imeonyesha kuwa chakula kikuu katika magereza nchini ni ugali na maharage. Mboga za majani, nyama, wali na matunda huliwa baadhi ya siku katika wiki.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ilibainika kuwa asimilia 59.2 ya wafungwa waliohojiwa walikiri kuwa chakula kinatosha kama kitasimamiwa na kuboreshwa huku asilimia 40 walikiri kuwa chakula hakitoshi.

Tume inapendekeza kuondolewa kwa matumizi ya mitondoo magerezani kwani hali hii imejitokeza zaidi katika mabweni ya wafungwa wa kunyongwa mfano gereza la Isanga, Ukonga, Uyui na Gereza la Mahabusu la Morogoro.

Tume inashauri upekuzi wa wafungwa kwa kuwavua nguo hadharani utafutiwe njia mbadala kwa vile utaratibu wa sasa unavunja haki ya faragha na staha ya mtu.

Aidha, kuna fursa ya kutembelewa na ndugu zao na kuonana nao ana kwa ana. Magereza yote yametayarisha sehemu maalumu na taratibu za kufuatwa wakati wafungwa na mahabusu wanapowasiliana na jamaa zao.

Msemaji Magereza
Hata hivyo, wiki iliyopita Msemaji wa Jeshi la Magereza, Mtiga Omari alisema kuwa jeshi lake limekuwa likipambana na vitendo hivyo viovu na kwamba wapo watu wengi wakiwamo raia na wafungwa ambao wamefunguliwa kesi za kuwasaidia wafungwa kumiliki simu gerezani.

Mtiga alisema jeshi hilo lina mambo mengi ambayo wananchi wanapaswa kuyajua, lakini atayazungumzia kwa ruksa ya Kamishina wa Magereza, Augustine Nanyaro.


MJUE VAN VICKER, MWIGIZAJI ANAYEPIGWA VITA NCHINI NIGERIA HIVISASA...


Huyu jamaa anaitwa JOSEPH VAN VICKER! Ni mwigizaji maarufu wa Movie za Kinigeria anayejulikana sana Barani Africa! Baba yake ni Mholanzi na mama yake ni Mghana. Baba yake alifariki Dunia wakati Van Vicker akiwa na umri wa miaka 6 na kuanzia hapo alilelewa na mama yake mpaka alipokuwa na uwezo wa Kujitegemea! Jamaa ameshanyakuwa Tuzo kibao za Filamu na pia inasemekana baada ya yeye kutoka kwao Ghana na kuhamishia kazi zake za Filamu nchini Nigeria na kukumbana na Ubaguzi mkali kwa wadau wa Filamu na hasa waigizaji wa Nollywood waliodhani aatawafunika na kweli 'AKAWAFUNIKA' kweli na hata waigiza maarufu wa kimume nchini humo kama vile RAMSEY NOAH, JIMMY IYKE na wengineo jasho linawatoka sasa...

Hobbies za huyu jamaa ni kucheza Football, Table tennis na kuogelea...

MCHEC VAN VICKER KWENYE KIPANDE HIKI SASA...

Thursday, September 29, 2011


Mwigizaji huyu anayependwa sana na wakina Dada ameshaoa jamani na amejaaliwa kupata watoto 3! Kwaiyo kama kuna siku ulikuwa na ndoto 'MBAYA' na yeye basi imekula kwako...

JAMAA PIA NI LULU KWENYE MATANGAZO YA BIASHARA, MCHEC HAPA...

KWA YALIYOTOKEA ZAMBIA JUZI NI MFANO WA KUINGWA NA VIONGOZI WOTE WA AFRICA...


Huyu ndie Rais mpya wa Zambia Mh. MICHAEL SATA, na hapa ni wakati anaapishwa juzi kushika Madaraka mapya ya kuiongoza nchi hiyo...

Na huyu ndie Rais aliyemaliza muda wake Mh. RUPIA BANDA.
RAIS mpya wa Zambia, Michael Sata aapishwa na kuahidi kupambana na ufisadi na umasikini nchini humo.
Akihutubia baada ya hafla ya kuapishwa, Sata ambaye ni kiongozi wa chama cha cha Patriotic Front (PF) ambaye pia anajulikana kwa umaarufu kwa jina la ‘King Cobra’ ameahidi kupambana na umasikini na ufisadi aliouita kuwa ni maradhi ambayo yanapaswa kupatiwa tiba.

‘King Cobra’, ameapishwa rasmi mjini Lusaka kuwa rais mpya wa nchi hiyo baada ya kushinda katika uchaguzi dhidi ya rais anayeondoka Rupiah Banda.Banda ambaye alikuwa aamini machoni mwake kwa kilichotokea, alitoa hotuba yakukubali matokeo hayo huku akiwa anabubujikwa na machozi mbele ya waandishi wa habari.

“Watu wa Zambia wamezungumza na lazima sote tusikilize," Banda alisema maneno hayo kwa hudhuni huku akiwa anafuta machozi baada ya kumaliza kutoa hotuba yake.Banda aliongeza kuwa, "Nikizungumza kwa nafsi yangu na chama changu, tunakubali matokeo. Sisi ni chama cha kidemokrasia na hakuna namna nyingine yeyote ile."

Habari zinasema kuwa, chama cha Movement for Multiparty Democracy (MMD) kilichokuwa kinaongozwa na Banda kimekuwepo madarakani nchini Zambia kwa miaka 20.

Sata ambaye anajulikana kwa umaarufu ‘King Cobra’, ni kiongozi wa chama cha Patriotic Front (PF) ambaye ana umri wa miaka 74, baada ya kuapishwa alisema kuwa, wawekezaji wa kigeni wanakaribishwa katika taifa hilo la Afrika lililo na utajiri wa madini ya shaba, ili mradi tu watii sheria za ajira nchini humo.

Sata ana ungwaji mkono mkubwa katika eneo hilo la uchimbaji madini ambapo amewalaumu wakurugenzi wa China kuwatumia vibaya, kuwanyanyasa na kuwapa malipo kidogo wafanyakazi nchini humo.

Zaidi ya asilimia 60 ya wananchi wa Zambia wanaishi chini ya kipato cha dola mbili kwa siku.Siku ya Alhamisi, kulikuwa na ghasia eneo la Kaskazini lenye migodi zilizofanywa na wanaounga mkono upinzani wakiwa hawana subra na matokeo ya Jumanne.

Matokeo hayo yalitangazwa huku majimbo saba yakiwa bado kura zao kuhesabiwa, lakini maofisa wa uchaguzi wamesema Banda hatoweza kumfikia Sata.Habari katika mitaa mbalimbali nchini humo, zinasema kuwa wasiwasi uliogubika matokeo hayo ulisababisha makelele huku wafuasi wa Patriotic Front wakishangilia ushindi wao.

Maelfu ya watu walifurika nje ya geti lenye ulinzi mkali wakipiga ngoma, wakipiga honi na kupeperusha bendera.

Tuesday, September 27, 2011

LEO KWENYE MAAJABU YA DUNIA


Huyu ni Mbwa mdogo tena wa ndani ya nyumba aitwae PUGGY mwenye umri wa miaka 8 aishie Stanford Hill hapa Central Londo. Mbwa huyu ni mdogo kwa umbo ila ndie Mbwa mwenye 'ULIMI' mrefu kuliko Mbwa wooote Duniani wanaoishi sasa! Ulimi wake una urefu wa inchi 4.5

SOMA HAPA CHINI, JINSI YA KUEPUKA KUWA MWAUME 'SURUALI'...
MWANAMUME ni kichwa cha familia, kwa maana ndiye kiongozi katika familia. Hakuna ubishi kuwa kiongozi akiwa wa hovyo, wengine watakuwa na wakati mgumu kuwa na maendeleo. Inasikitisha kwamba kuna watu wako kwenye ndoa wanatesana badala ya kupeana raha. Kuna wanaume wanawatesa wake zao, kisa wana vimada nje ya ndoa. Kuna wanawake nao wanao wanaume wengine, ndani ya ndoa ni jeuri tupu, ukweli ni kwamba haya yote ni ujinga. Katika maisha mume na mke wanapaswa kufahamu kuwa wanalo deni la kupendana. Katika ndoa ni lazima uwe makini na kauli na matendo yako. Usipendelee kuongea kauli ambazo ukiambiwa hautazifurahia. Maisha sahihi katika ndoa ni pamoja na kila mmoja kujiona kuwa analo deni la kumtendea mwingine lililo jema. Je mkeo unamtendea jema gani? Kuna wanaume wengi, kwa nje wanaonekana wazuri, lakini wanawatesa sana wanawake zao. Nimekuwa nikitoa ushauri wa ana kwa ana na kuendesha semina kila jumamosi za masuala ya ndoa, kati ya kero kubwa katika ndoa ni wanaume kuwa na roho mbaya, wanawanyanyasa wanawake kwa matendo na hata wakati mwingine kuwapiga. Kasi ya wanaume kuwapiga wanawake imepungua huenda ni kwa hofu ya sheria, bado kuna wanaume wamekuwa wanyanyasaji, kwa mfano wa kauli chafu, anarudi nyumbani amelewa halafu analazimisha tendo la ndoa wakati ananuka jasho. Hii si sahihi hata kidogo. Mwanamume kurudi nyumbani umeshashiba si hekima, kurudi nyumbani usiku wa manane kwa sababu umetoka kwenye uchafu wako. Wengine wanapokuwa wametoka nyumba ndogo, wanaingia kwa wake zao kwa fujo na makelele, mbona nyumba chafu!!! Eeeh utatoka hapa!! Yamekujaje haya, kumbe anafanya hivyo mke asiweze kuhoji mbona unanuka harufu ya kondom, au mafuta ya kike nk. Unajiona mjanja, kumbe ni ujinga. Kuna wanaume wako tayari kuwaendeleza nyumba ndogo,si wake zao. Huu ni upumbavu. Ndugu yangu vipi una akili kweli? Huna. Angalia vizuri matendo yako. Ni aibu mzazi kuruhusu watoto wake kutosoma au kutofanya mambo mengine ya maendeleo. Mwanamume kweli (si mwanamume suruali), hufanya mikakati ya kuhakikisha watoto na familia yake inakuwa na maisha yanayofaa, wanakula, wanavaa, wanasoma na wakati fulani kupata nafasi ya kuzungumza na watoto au mkewe. Je wewe mara ya mwisho kujadiliana na mkeo ni lini? Chunga sana maisha yako, fainali uzeeni. Unawekeza fedha kwenye gesti, unawekeza fedha kwenye ulevi na anasa, jua unajiharibia mwelekeo wa maisha yako mwenyewe. Jua kwamba utavuna unachopanda. Haiwezekani, upande bangi utarajie kuvuna mpunga!!! Mwanamume pia unapaswa kuwa makini katika suala zima la afya; ni makosa kwa mfano kula tu ili mradi, bali unatakiwa kujua hiki nakula kwa ajili ya nini. Hivi sasa kuna kasi kubwa ya wanaume wenye tatizo la nguvu za kijinsia, mojawapo ya sababu ni ulaji usiofaa. Zipo sababu zingine kama vile kujichua, mikwaruzo katika mahusiano, kuwa na mpenzi asiyejua mambo, uvutaji sigara na ulevi au kufanya mazoezi kwa muda mrefu kisha kuacha, kwa asilimia kubwa vyakula vinachangia. Ziko dawa za kutibu kabisa tatizo la nguvu za kijinsia kama nilivyozungumzia hivi karibuni, huna sababu ya kulia, badala yake unapaswa kuchukua hatua, kwani ushindi haupatikani kwa kulia, bali kwa kuchukua hatua kupambana na kile ambacho kinakusumbua. Amka ndugu yangu, cha msingi katika maisha ni kupambana na kile kinachokusumbua, kwa hakika mwisho utashinda, na ndoa yako itakuwa nzuri. Kuepuka kuitwa �mwanamume suruali� unapaswa kuwa mwanamume kweli unayejua majukumu yako na kuyatenda kwa vitendo, unapaswa kuwa imara kwa kila kitu kuanzia uchumi hadi mahaba, tafiti zinaonyesha kuwa wanawake wanahitaji wanaume rijali, si goigoi!!! Si kwamba kwao hakuna chakula, ndio maana amekubali kuwa nawe, wanahitaji mengine na hilo pia, kama ambavyo wanaume wanahitaji!!!

HUYU NDIE MCHEZAJI WA KWANZA AFRIKA MASHARIKI KUCHEZA SOKA ULAYA...


Huyo bwana anaitwa SUNDAY RAMADHANI MANARA aka 'Computer' aliyezaliwa miaka 54 iliyopita mjini Kigoma mahali ambapo palikuja kuwa chimbuko la wachezaji wengi nyota kama akina Hamis Askari, Aloo Mwitu, Athuman Juma, Juma Kampala, Abeid Mziba, Makumbi Juma na wengineo.
Mkongwe huyo, ambaye ndugu zake wawili nao walikuwa wanapiga soka yaani Kitwana Manara kaka yake na mdogo wake Kasimu Manara kwa sasa anapatikana maeneo ya Temeke, jijini Dar es Salaam.


MAISHA YA UTOTONI KATIKA SOKA
Sunday anakumbuka maisha yake ya utotoni alianza kuchezea Young Kinya ambayo ilikuwa kama timu ya watoto wa Yanga ingawa ilikuwa kama inajitegemea zaidi na ilikuwa inafanya mazoezi nje ya viwanja vya Kaunda na ilikuwa ukitoka pale unasogea kidogo unakwenda Afrikan Boys ambayo ilikuwa ni timu ya pili ya Yanga na mwanzoni mwa miaka ya 1970 Sunday na wenzie akina Awadhi Kessy, Douglas, Shabaan Ufunguo, Mohamedy Ugando walipandishwa kuichezea Yanga ya wakubwa chini ya kocha Profesa Victor Stanculescu na huko waliwakuta kina Elias Michael, Mohammed Msomali, Hassan Goboss, Boi Iddy, Athuman Kilambo, Maulidi Dilunga, Badi Salehe, Leonard Chitete na wengineo.

MALEZI YAKE KWA STANCULESCU
Sunday, ambaye binafsi anakiri kuwa hajui jina la mashine hiyo yenye kufanya kazi vizuri alipewa na nani zaidi ya kukumbuka tu ni mwaka 1975 alipotoka Zanzibar baada ya kuwapiga Simba mabao 2-0 ila anakubali kuwa maisha waliyokuwa wanalelewa na Mzungu huyo yalimfanya aipende sana Yanga kuliko timu nyingine yeyote ikiwamo Taifa Stars, ambayo walikuwa wachezaji takribani saba, ambao ni kipa Elia Michael, Athuman Kilambo, Hassan Gobboss, Abdulhaman Juma, Kitwana Manara, Gibson Sembuli na yeye mwenyewe.
Ushirikiano ulikuwa mkubwa na ulisababisha kuwa mara zote ni furaha tupu ndani ya mitaa ile ya Jangwani hadi mwaka 1973 ambapo Simba ilifuta uteja kwa kuwafunga bao 1-0 lililowekwa kimiani na nahodha wa Simba wakati huo, Haidar Abeid �Muchacho�.

SUNDAY MANARA NA SIMBA
Sunday anasema mara zote alizokuwa akikutana na Simba alikuwa anawaua tu bila masihara, mwaka 1971 Simba ilifungwa mabao 2-0 na moja alifunga yeye na jingine alifunga Maulid Dilunga, mwaka 1974 mechi ya kihistoria ambayo ilipigwa mjini Mwanza katika Uwanja wa Nyamagana, Simba ilifungwa mabao 2-1, yaliyofungwa na Adam Sabu kwa upande wa Simba kabla ya Gibson Sembuli kufunga dakika ya 87 na Sunday Manara kushindilia msumali wa mwisho dakika 30 za nyongeza.
Mechi nyingine ilikuwa ni fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki iliyopigwa mjini Zanzibar katika Uwanja wa Amaan na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, huku goli la kwanza likifungwa na Sunday Manara la umbali wa zaidi ya mita 25 na kusababisha utata mkubwa kwa manazi wa Simba wakimtuhumu kipa wao Athuman Mambosasa kuwa aliachia makusudi au alipewa kitu kidogo na bao la pili lilifungwa na Gibson Sembuli kama kawaida yake kwa shuti kali sana.
Mbali na kuifunga Simba mara zote hizo, Sunday pia alikuwa ni rafiki mkubwa sana wa kipenzi cha Simba, Abdallah King Kibaden Mputa ambaye kwa sasa ni meneja wa Simba.
Sunday pia alioa binti wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba, mzee Hassan Haji ambaye ni baba mkubwa wa Mohammed Mkweche aliyekuwa beki maarufu wa Pan African.
Simba pia ndio waliofanikisha mpango mzima wa Sunday Manara kwenda kucheza soka la kulipwa nje ili atoe balaa la wenyewe kufungwa na mtu huyo, huo ndio uhusiano wake na Simba maarufu kama Lunyasi

KUVUNJIKA KWA YANGA KUZALIWA PAN
Sunday akizungumza kwa masikitiko makubwa na bila kumung�unya maneno anamtupia lawama kubwa kocha raia wa Zaire wakati huo, Tambwe Leya kuwa baada ya kutolewa na Enugu Rangers ya Nigeria katika mashindano ya Afrika aliwatuhumu wachezaji nyota akina Sunday, Omary Kapera, Sembuli na wengineo kuwa wameihujumu timu hadi kusababisha kufungwa hivyo wanachama kwa hasira wakawafukuza viongozi wote wakiongozwa na mzee Tabu Mangara na Shiraz Sharif na kuwekwa viongozi wengine ambao waliwataka wakiri makosa.
�Kwa kuwa hatukujua kosa letu, tukaondoka na kuelekea Nyota Afrika ya Morogoro na baadaye tukarudi Dar es Salaam na kuunda timu inaitwa Pan mwaka 1976,� anasema.

SUNDAY MANARA NA SOKA LA KULIPWA

Mwaka 1977 Sunday alitimkia Uholanzi kupiga soka la kulipwa na alikuwa mchezaji wa kwanza Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kwenda kucheza katika ligi kubwa Ulaya katika timu ya Heracles ambayo ipo hadi sasa katika ligi hiyo na huko alikutana na watu kama akina Jaan Rep, Ruud Krol, Johan Neeskens, Johan Cruyff ,Van Hangem na wengineo. Alikaa huko mpaka mwaka 1979 alipotimkia nchini Marekani ambako walikuwa wameanza mipango ya kukuza soka nchini kwao.

TENGA KAJIFUNGIA NA FIKRA ZAKE
Sunday akizungumzia soka la Tanzania anamshushia lawama nzito Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Leodegar Tenga kuwa analipeleka soka kuzimu na kuwa hahitaji ushauri kwa watu ambao anajua kabisa kuwa wamecheza soka kwa upeo mkubwa na soka wanalielewa kama yeye.

�Tenga hapendi kukosolewa sasa mawazo mapya atayapata wapi? Namshauri kama mdogo wangu aitishe mdahalo wa kitaifa tuzungumzie soka, tupo tunaojua matatizo ya soka si hao wenye vyeti na soka hawalijui,� anasema Computer ambaye kwa sasa yuko mbioni kuwa na Academy yake ambayo itakuwa mfano wa kuigwa nchini

SOKA LA ZAMANI NA SASA
Computer anasema viongozi wa zamani walikuwa na mapenzi makubwa na viongozi wenzao wa timu nyingine na wachezaji wa upande mwingine pia wachezaji walikuwa wanapendana nje ya uwanja, upinzani ilikuwa ndani ya uwanja.

Sunday, ambaye ni mpenzi wa Barcelona ya Hispania anawasifia wachezaji kama Mbwana Bushiri, Emil Kondo na John Lyimo kuwa walikuwa na vipaji vya hali ya juu, ingawa anakiri kuwa hata sasa wapo wenye vipaji lakini wameshindwa kuvumbuliwa.


Website counter