Siku ya onyesho yaani jana Ijumaa nilikutana mwanamuziki maarufu wa CONGO FERRE GOLLA aliyeko nchini kwa ziara fupi ya maonesho yake mawili mchana hotelini kwake MOVENPICK tukaongea na ndipo aliponiambia anataka kwenda sehemu kula Nyama Choma basi nikamwambia nampa 'Ofa' ya chakula cha mchana kwenye PUB yangu ya KINYAIYA'S PUB iliyoko Kinondoni nyuma ya Mango Garden nae akakubali na hapa kwenye picha ni wakati tunatoka PUB baada ya 'Msosi' wa nguvu na yeye anaelekea Hotelini kwake kupumzika kusubiri Concert yake ya usiku ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee Hall Upanga jijini Dar...
Naaam sasa hapa ni ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee Hall, mimi nilikuwa MC wa Onesho lake la jana na hapa ni wakati ambao baada ya wanamuziki wake kupanda jukwaani nilimwita FERRE GOLLA mbele ya jukwaa na kumtambulisha rasmi kwa wapenzi wa Burudani waliofurika ndani ukumbi huo ili awasalimie...
Nae bila hiyani akawasalimia watu kwa kiswahili chake kibovu na kuwaomba ushirikiano kuanzia kuimba wote na kucheza wote vilevile, ilikuwa balaaaa nakwambia...
Yaaap kazi ikaanza rasmi Stejini ambapo FERRE GOLLA aliporomosha 'Sebene' la kufa Ngamia kama si m2 daaah...
1 comment:
Ben mbona unarudia picha
Post a Comment