Saturday, September 25, 2010

KITAANI WIKI HII....


Hapa nikiwa na Mchezaji wa kiungo wa wekundu wa Msimbazi timu ya SIMBA na timu ya Taifa ABDULHALIM HUMUD, tulipokutana jana kwenye duka la nguo na vifaa vya michezo la ZIZZOU maeneo ya Victoria jijini Dar...

Huyu ni Paka wangu niliyempenda sana aitwae ROCK ambaye amekufa juzi baada ya kula kitu chenye sumu! Mimi huwa napenda sana wanyama na ninafuga pia MBWA na KASUKU ambaye anaongea kama Binadamu na ndio furaha yangu kila ninapowaona na kuongea nao coz wananielewa kila ninachowaagiza! Nitamkumbuka Paka wangu huyu kwa Desturi yake ya kulala na Mdoli wake pembeni na kama ukiuficha huo Mdoli basi atapiga sana kelele mpaka uurudishe ndio atanyamaza! Buriani ROCK wangu nitakumic saanaaaa...

Hii ni jana nilipokwenda kumsalimu Swaiba wangu MAIMARTHA ambae bado yuko ndani mpaka 40 ya marehemu mchumba wake P-DIDDY iishe ndio ataanza kufanya kazi na ndio maana kwenye kipindi changu sikuizi mnaniona mwenyewe LUNINGANI...

Nikiwa na MAPACHA wanaofanana kama Chupa za Bia waitwao HASSAN na HUSSEIN. Hawa jamaa wana tabia tofauti, huyo aliyeko kulia ni mpole saanaaa na hana makuu ila uyo aliyeko kushoto ni balaa kwa utundu na fujo za kila aina na ndie rafiki yangu mkubwa kuliko huyo mpole....

Hapa nikiwa na Mapacha pamoja na JACK PEMBA tukifurahia maisha kiaina...

2 comments:

Ima (The Designer) said...

Nice Photo naona uko na mapacha wazee wa kura bata.

Anonymous said...

MASKINI MAIMARTHA NAONA HATA TABASAMU SIO LILE TULILOLIZOEA MUNGU AMJAALIE IMANI NA KUSAHAU.ILA WENZETU WAZUNGU WANA UTAMADUNI WA KUFANYA COUNCELLING (SIJUI NDIO INAANDIKWA HIVYO) NA WANASAIKOLOJIA ILI KUWAWEKA SAWA WAFIWA KIAKILI. BEN HEBU MCHEKI KAMA UNAONA ANA MAWAZO SANA MTAFUTE MWANA SAIKOLOJIA WANAPATIKANA HASA KWENYE VYUO VIKUU HUWAGA NI MA DEAN OF STUDENTS WAMESOMEA MAMBO HAYA.TUNAMSUBURI KWA HAMU KWENYE SHOW YENU

Website counter