Tuesday, July 6, 2010

WAJAMENI NAWAULIZA ENYI WANAWAKE NA WASICHANA, ETI 'HENNA' HUPAKWA WAKATI GANI HASAA...


Sie vidume twataka kujua kwa iyo Henna inapakwaga wakati gani hasaa ili kama ukiona mwanamke amepakwa aina flani ya henna basi tujue kama huyo katoka kuolewa ama bado mwali ama pengine kafiwa! Maana nimeshaona sehemu zingine watu wakifiwa wananyoa vipara bila kujali wee ni mwanamke au mwanaume kwenye iyo Familly! Sasa tuambieni bwanaaa....

3 comments:

Anonymous said...

Hina bwana ni pambo la mwanamke katika nchi nyingi lakini mimi ntakwa mbia kwa sisi wa tz wa pwani ni pambo la mwanamke hasa aliokuwa na mume ni pambo la kumpambia mumewe ndo mana utaona mabiharusi hupambwa kwa hina siku ya harusi na mara nyingi bi harusi hupakwa nakshi nyingi sana yani mgongoni wengine kiunoni mikono mpaka juu na miguu mpaka magotini. mwanamke mwenye mume mara nyingi hupaka kiasi tu mikononi miguuni Japo style ile ya biharusi anaweza kupaka pia wakipenda.
Watoto wadogo nao hurembwa hina hassa kwenye sherehe au sikukuu.
Msichana mwari aliyekwisha vunja ungo haruhusiwi kupaka hina japo siku hizi utawaona wamejiremba kama ndo wanatoka kuolewa upashkuna tu kujitukanisha maana hina unampakia mume we mwari unampakia nani si ndo unaonyesha watu kuwa una BWANA huko nje unayempakia?! toka zama haya mambo ya ma B.F yapo lakini watu walikuwa wanafanya siri na ndo utamu wake unapopatikana hapo lakini mila zimevuliwa nguo siku hizi mpaka msichana anahesabiwa alikuwa na nani na nyani!
P.T.O (utajaza umechokoza nyuki! LOL)

Anonymous said...

Naendelea....

Mimi binafsi tulikuwa tunapakwa hina nyumbani siku za sikukuu na mzee wetu anatoa pesa kabisa mtu anaturemba enzi zile mtaa wa tandamti/Lumumba kwa Ma Laki maaarufu kupaka hina na wanja(sio piko) na siku nyingine nyumbani wenyewe tulikuwa tuna M-Hina tunakausha tunatwanga tunajishaua kujipakapaka hatuulizwi kitu na mtu, Tulipokuwa tu tukapigwa stop tena kupaka hina labda ujitie kucha tu mpaka tumeolewa ndo tukapakwa tena yaani unajiona unavyomeremeta unajiona mpyaa kabisa kwa vile hujazowea kujiona vile yaani unajiona aaah kweli mi leo bi harusi.
Sasa ikaja kwa huyu bwana huku hina anapenda sana ila nimepigwa stop mambo ya kuchorwa viunoni na migongoni yaani mambo ya kuvulia wanawake wenzio nguo hataki anasema ndo wanavyoanza kusagana sijui, eti kweli?!
au ndo mnavyodanganyana huko?!
basi hiyo ndo story yangu ya hina bwan ben, nikutumie picha yangu ya harusi?!

KINYAIYAS ENTERTAINMENT said...

yaaa kama unaweza nitumie iyo picha yako ya Harusi tuione! ben.

Website counter