Wednesday, July 28, 2010

KOCHA MPYA AIVUNJA BRAZIL YOOOTE...


Kocha mpya wa timu ya Taifa ya BRAZIL MANO MENEZES aliyechukua nafasi ya Capt DUNGA amekivunja kikosi chooote kilichokuwepo kwenye kombe la Dunia nchini Africa ya kusini kasoro Dan Alves, Ramirez na Robinho na kuchukuwa vijana watupu na wengi wao wakiwa wanacheza kwenye ligi ya nyumbani Brazil na kusema kuwa hana haja ya kuwatumia tena mastaa hao maana wana nyodo kuanzia mazoezini hadi nje ya uwanja na kujifanya ni 'wakubwa' kuliko Kocha wao! Aaahaaaa na ndio maana Brazil ya miaka ya karibuni ni mbovu na wala hawachezi lile soka lao la kuvutiaaaa, yaap kama ivyo safi sana fukuza woote chukua vijana anza upya, waache wakae na 'mipesa' yao inayowandisha kichwa alaaah, watu wanataka vijana wa kazi bwana na sio nyodo apa...

No comments:

Website counter