Sunday, July 25, 2010

JAMANI TUMSHAURI KIJANA MWENZETU...

Habari kaka Ben naitwa 'G' kwa kifupi, naipenda Blog yako na mimi ni shabiki yako mkubwa na haswa kwa namna unavyojua kutangaza 'LUNINGANI', na ndio maana nimeamua kuomba ushauri kwako na kwa wadau wengine wa Blog yako ingawa nisingependa unitaje jina langu wala kuchapisha email yangu plz plz! Tatizo langu ni kwamba mimi ni mchaga mzaliwa wa Marangu Kilimanjaro na wakati nikiwa kijijini kabla sijaja mjini niliwahi kuwa na Girlfriend uko kwa muda mwingi ila baadae tuliacha na baada ya hapo nikahamia Dar kutafuta 'Life' na baadae nikakutana na msichana flani aliekuwa anaishi jirani na Duka langu maeneo ya Kinondoni Moscow, tukapendana sana na sasa tuna miaka 3 na nimeshamchunguza tabia zake nimeona anafaa kuwa 'Mke' na tunataka kuoana kabsaa, sasa la ajabu nilipompigia simu Mama yangu kule Marangu kumweleza habari ya kwenda kumtambulisha 'mgeni' wangu kwake akawa mkali na kuniambia hataki kusikia huo 'upuuzi' wangu wa kwenda na mtu wkt yeye anaamini kwamba Mwanamke ninaetakiwa kumwoa ni yule alieko Bush ingawa anajua kabisa tulishaacha miaka mingi sasa, eti hawa wa mjini ni matapeli tu! Tukagombana sana kwenye simu lakini wapi hataki niende na mtu kule Bush kuongea nae, labda niende peke yangu! Baba yangu alishafariki kitambo kwaiyo kabaki yeye kwenye Boma letu, sasa naomba ushauri jamani nifanyaje apo, niko njia panda kaka Ben...

1 comment:

Anonymous said...

Pole sana kijana najua upo kwenye wakati mgumu sana,lakini kinachotakiwa hapo ni dialogue, nenda kwa mama peke yako na mkayaongee kwa kina.

Usije ukachukua maamuzi alafu baadaye mambo yakakuaribikia na ukajuta, naamini wazazi wetu wanatupenda sana na wanataka sisi watoto tuwe na maisha bora.

Kakae na mama na uongee na kama bado ankuwa na jazba wewe vuta subra

Na kuhusu huyo binti wa kijijini lazima akapime afya kwanza ndio umsikilize vinginevyo utakanyaga mto.

Pole fanya maombi na roho mtakatifu atakuongoza njia iliyo salama.

Pole sana

Mdau Nico

Website counter