Tuesday, September 27, 2011

SOMA HAPA CHINI, JINSI YA KUEPUKA KUWA MWAUME 'SURUALI'...




MWANAMUME ni kichwa cha familia, kwa maana ndiye kiongozi katika familia. Hakuna ubishi kuwa kiongozi akiwa wa hovyo, wengine watakuwa na wakati mgumu kuwa na maendeleo. Inasikitisha kwamba kuna watu wako kwenye ndoa wanatesana badala ya kupeana raha. Kuna wanaume wanawatesa wake zao, kisa wana vimada nje ya ndoa. Kuna wanawake nao wanao wanaume wengine, ndani ya ndoa ni jeuri tupu, ukweli ni kwamba haya yote ni ujinga. Katika maisha mume na mke wanapaswa kufahamu kuwa wanalo deni la kupendana. Katika ndoa ni lazima uwe makini na kauli na matendo yako. Usipendelee kuongea kauli ambazo ukiambiwa hautazifurahia. Maisha sahihi katika ndoa ni pamoja na kila mmoja kujiona kuwa analo deni la kumtendea mwingine lililo jema. Je mkeo unamtendea jema gani? Kuna wanaume wengi, kwa nje wanaonekana wazuri, lakini wanawatesa sana wanawake zao. Nimekuwa nikitoa ushauri wa ana kwa ana na kuendesha semina kila jumamosi za masuala ya ndoa, kati ya kero kubwa katika ndoa ni wanaume kuwa na roho mbaya, wanawanyanyasa wanawake kwa matendo na hata wakati mwingine kuwapiga. Kasi ya wanaume kuwapiga wanawake imepungua huenda ni kwa hofu ya sheria, bado kuna wanaume wamekuwa wanyanyasaji, kwa mfano wa kauli chafu, anarudi nyumbani amelewa halafu analazimisha tendo la ndoa wakati ananuka jasho. Hii si sahihi hata kidogo. Mwanamume kurudi nyumbani umeshashiba si hekima, kurudi nyumbani usiku wa manane kwa sababu umetoka kwenye uchafu wako. Wengine wanapokuwa wametoka nyumba ndogo, wanaingia kwa wake zao kwa fujo na makelele, mbona nyumba chafu!!! Eeeh utatoka hapa!! Yamekujaje haya, kumbe anafanya hivyo mke asiweze kuhoji mbona unanuka harufu ya kondom, au mafuta ya kike nk. Unajiona mjanja, kumbe ni ujinga. Kuna wanaume wako tayari kuwaendeleza nyumba ndogo,si wake zao. Huu ni upumbavu. Ndugu yangu vipi una akili kweli? Huna. Angalia vizuri matendo yako. Ni aibu mzazi kuruhusu watoto wake kutosoma au kutofanya mambo mengine ya maendeleo. Mwanamume kweli (si mwanamume suruali), hufanya mikakati ya kuhakikisha watoto na familia yake inakuwa na maisha yanayofaa, wanakula, wanavaa, wanasoma na wakati fulani kupata nafasi ya kuzungumza na watoto au mkewe. Je wewe mara ya mwisho kujadiliana na mkeo ni lini? Chunga sana maisha yako, fainali uzeeni. Unawekeza fedha kwenye gesti, unawekeza fedha kwenye ulevi na anasa, jua unajiharibia mwelekeo wa maisha yako mwenyewe. Jua kwamba utavuna unachopanda. Haiwezekani, upande bangi utarajie kuvuna mpunga!!! Mwanamume pia unapaswa kuwa makini katika suala zima la afya; ni makosa kwa mfano kula tu ili mradi, bali unatakiwa kujua hiki nakula kwa ajili ya nini. Hivi sasa kuna kasi kubwa ya wanaume wenye tatizo la nguvu za kijinsia, mojawapo ya sababu ni ulaji usiofaa. Zipo sababu zingine kama vile kujichua, mikwaruzo katika mahusiano, kuwa na mpenzi asiyejua mambo, uvutaji sigara na ulevi au kufanya mazoezi kwa muda mrefu kisha kuacha, kwa asilimia kubwa vyakula vinachangia. Ziko dawa za kutibu kabisa tatizo la nguvu za kijinsia kama nilivyozungumzia hivi karibuni, huna sababu ya kulia, badala yake unapaswa kuchukua hatua, kwani ushindi haupatikani kwa kulia, bali kwa kuchukua hatua kupambana na kile ambacho kinakusumbua. Amka ndugu yangu, cha msingi katika maisha ni kupambana na kile kinachokusumbua, kwa hakika mwisho utashinda, na ndoa yako itakuwa nzuri. Kuepuka kuitwa �mwanamume suruali� unapaswa kuwa mwanamume kweli unayejua majukumu yako na kuyatenda kwa vitendo, unapaswa kuwa imara kwa kila kitu kuanzia uchumi hadi mahaba, tafiti zinaonyesha kuwa wanawake wanahitaji wanaume rijali, si goigoi!!! Si kwamba kwao hakuna chakula, ndio maana amekubali kuwa nawe, wanahitaji mengine na hilo pia, kama ambavyo wanaume wanahitaji!!!

No comments:

Website counter