Saturday, September 10, 2011

JAMANI 'WAMACHINGA' MPAKA ULAYA WAPO ILA KWA UTARATIBU MAALUM...


Jamani msidhani 'WAMACHINGA' wapo africa tu ila hata uku Ulaya pia wapo tena wa kumwaga sema wapo kwenye maeneo yaliyopangwa tu, sasa tatizo liko kwa wamachinga wa kwetu Africa wakipangiwa sehemu zao ili uharibifu wa mazingira upungue ni vita daaah! Yaani sisi mpaka tukae sehemu kwa utaratibu itachukua muda sana nakwambieni, na hapo kwenye picha msione NIMENUNA ni kwa sababu kuna Mturuki wa Bucha kaniulizia kuku wa 'Kiswahili' kwakua kaniona mie Mwafrica wkt mie nilitaka kuku wa Kizungu ambaye analainika 'Viungo' Fasta aaaagh...

Kuna pia wauza simu kama mnavyoona na tena wanajua kupiga 'DEBE' hao 'Ova' kariakoo duuuh...

Aaah mbona mambo mulemule 2 jamani...

Hii sehemu inaitwa BRIXTON, ipo katikati ya hapa London ila mtaa tu umetengwa kwa wamachinga pekee na wauza Nyama...

1 comment:

Anonymous said...

wa kiswahili ndiyo mzuri kaka wa kichaga yaan yupo real mabroiler mabaya hayo yana machemical nyingi mpike tu ataiva.hata viungo weka tu me nitakuja kula,halafu no yako ya uk hiyo mbn haipatikani hata msm haziendi nikituma

Website counter