Friday, November 12, 2010

JAMANIII EEEH NAULIZA IVII...


Waswahili sikuzote wanasema kuuliza sio ujinga, sasa mie nawauliza nyie wadau wa Blog hii, ivi kweli kuna haja ya kisiwa kidogo kama ZANZIBAR kuwa na makamu wawili wa Rais jamani? Na je ina maana CCM ya DK SHEIN 'hawamuamini' Makamu wa kwanza wa Rais MAALIM SEIF mpaka wateuwe mwingine kutoka kwao Balozi SEIF IDD kuwa Makamu wa pili wa Rais? Nomeni majibu yenu sanifu waungwana maana....

2 comments:

Anonymous said...

Hii biashara wliishaichemsha zamani,kungekuwa na raisi mmoja tu bila kujali lazima atokee wapi.

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Nijuavyo mimi hayo yalikuwa ni mojawapo ya mambo waliyokubaliana katika ule mwafaka uliokuwa na lengo la kumaliza mzozo wao wa kisiasa.

Kuwa na makamu wawili nadhani inaonyesha kwamba CCM hawakuwa na imani na Maalim (hawapendi serikali ya mseto) na pengine walikubali tu kwa shingo upande. Sitashangaa kama Maalim atakuwa tu pale kama "kivuli" bila mamlaka wala "meno" ya kupitisha maamuzi yo yote yenye kutathmini na kuathiri mwelekeo wa nchi. Na walipa kodi ndiyo wanaishia kubebeshwa mzigo usio wa lazima. Wanasiasa na siasa zao ati!

Website counter