Tuesday, November 16, 2010

NAKUHAKIKISHIA MMOJA WAPO KATI YA HAWA NDIE ATAKUWA WAZIRI MKUU WA 'NJI' HII...


Huyu ni Mh JOHN POMBE MAGUFULI, ni mmoja kati ya mawaziri wachache nchini wenye uwezo mkubwa kiutendaji, na ni Waziri 'KIRAKA' ambaye ukimuweka wizara yoyote ile anaweza kuimudu ipasavyo, sio kama wengine wanamudi wizara 'flani' 2 na endapo utamuhamisha 2 basi atachemka...

Anaitwa MIZENGO KAYANZA PETER PINDA, ni waziri mkuu wa sasa wa serikali iliyopita na ni mzuri pia kiutendaji na huwa ananifurahishaga anapokuwa Bungeni hasa pale anapojibu maswali ya 'Ana kwa ana' kutoka kwa wabunge, anastahili kuendelea na wadhifa wake ila inategemea vilevile...

Anaitwa SAMUEL SITTA, yeye alikuwa Speaker wa Bunge la Tanzania lililopita! Ninachompendea mzee huyu ni jinsi alivyo na msimamo kwenye ishu muhimu bila kumuogopa m2 yoyote kwa jambo analoliamini kichwani mwake! Alilichangamsha Bunge lililopita kwa kulifanya liwe la uwazi zaidi kuanzia Mijadala mpaka Hoja na anachukiwa zaidi na Mafisadi kutokana na misimamo yake yakinifu, na kwakweli anastahili 'Uwaziri mkuu' safari hii hasa baada ya 'Chama' kumwaga kwenye uteuzi wa kuwania Uspika wa Bunge hili la sasa ambalo Mama ANNA MAKINDA ameutwaa kiulainiiii...

No comments:

Website counter