Friday, November 12, 2010

HATIMAYE KILIO CHA 'MAMA YETU' KIMESIKIKA DAAH...


Hatimaye kilio chetu sie wenye nafasi ya 'Kuchonga' kimesikika baada ya Serikali kuamua kufanya mpango wa kumtibia aliyekuwa mkuu wa Wilaya mkongwe nchini mama HAWA NGULUME na hata ikiwezekana kumpeleka nje ya 'NCHI' daah! Sasa mie najiuliza iweje Serikali yetu mpaka ipigiwe kelele kuanzia za mgonjwa mwenyewe mpaka kina sie 'Wachongaji midomo' ndio mstuke kwamba mtumishi wenu ana hali mbaya jamaniiii?Huyu mgonjwa Mama NGULUME mwenyewe alishawahi kwenda Muhimbili na kugandishwa kwenye foleni masaa kibao na tena Manesi wanampita 2 mpaka mwenyewe akaamua kujiendea kupoza maumivu yake kwenye Hospital za Binafsi wakati ni mtumishi wa Serikali kwa miaka zaidi ya 17 akiongoza Wilaya mbalimbali tofauti nchini? Yaani mpaka apige kelele kwenye vyombo vya habari ndio mumsikie jamani? Kwakweli ni aibu sanaa basi 2 loooh...

No comments:

Website counter