Monday, October 11, 2010


Leo ilikuwa ni siku ya huzuni kwetu sisi waandishi wa habari na utangazaji baada ya kumpoteza mwenzetu ABDALLAH RAMADHANI aliyekuwa akifanya kazi katika Television ya CHANNEL TEN ya jijini Dar. Marehemu alifariki juzi Jumamosi baada ya kupata ajali mbaya alipokuwa akirudi nyumbani kwa njia ya Barabara akitokea nchini MSUMBIJI baada ya gari aliyokuwa akiendesha kupinduka mara 4 baada ya kupasuka Tairi ya mbele na wakati huo yeye akiwa kwenye kona kali. Nitamkumbuka marehemu kwa tabia yake ya aibu kwani kama hajakuzoea hawezi kujiachia na wewe kiivyo ila akikuzoea basi utamkoma kwa utani wake! Mungu ailaze roho yake peponi, AMEIN...

Hapa mkewe akiwa haamini kwamba safari ya mumewe mpenzi ndio imefikia TAMATI daah...

Akikumbatia maiti ya mumewe na kulia kwa uchungu huku akimfikiria mtoto wao mdogo atakaekosa mapenzi ya babake! Maskini mtoto nae alikuwa akicheza na wenzake bila kujua kinachoendelea ila muda ukifika atakuja kufahamu na kuikumbuka siku hii ya leo, ilikuwa ni Huzuni sanaa kwakweli...

Kazi ya mungu haina makosa, buriani DULLAH, tutakukumbuka daima rafiki...

No comments:

Website counter