Nilikuwa MC wa Uzinduzi huo wa kufa mtu wa Album ya 6 ya FM ACADEMIA iitwayo 'VUTA NIKUVUTE' na hapa nikitoa mwongozo wa shughuli huku nikishuhudiwa na kuazia kushoto ni Meneja masoko wa Zain Mr KELVIN TWISSA, akifuatiwa na Mama mwenyekiti wa Bia ya HEINEKEN TANZANIA Bi BENADICTA RWEGEMALILA na Mkurugenzi mwanzilishi wa Fm Academia mzee FELICIAN MUTA ambaye ndie aliimzisha bendi hiyo enzi zile za miaka ya 90 na kuipa jina la FM ikiwa ni kifupi cha majini yake! Sasa kwa wasiojua habari ndio hiyo, sio unajua majina ya vitu alafu maana yake hujui...
Waimbaji nguli wa FM ACADEMIA kuanzia kushoto ni JOSE MARA, KING BLAISE, BEN KINYAIYA na PABLO MASAI...
Nikiwa na mwanamuziki nyota wa Kenya NAMELESS na wanenguaji wake ambao walikuja nchini kuwasindikiza Fm Academia kwenye uzinduzi wao...
No comments:
Post a Comment