Friday, September 17, 2010

HAWA NDIO WAGENI WANGU WALIOKUWEPO KATIKA KIPINDI CHANGU CHA LIVE CHA JUMAMOSI ILIYOPITA TBC1...


Mgeni wangu wa kwanza katika kipindi changu cha Jumamosi iliyopita TBC1 alikuwa ni huyu bibie JAQ WOLPER ambaye ni mwigizaji maarufu wa kike wa Filamu nchini, mashabiki walikuwa LIVE studio walimfurahia ingawa walimuuliza maswali mengi mpaka akataka kukasirika ndipo nikamkumbusha kwamba kipindi changu ni Live kwaiyo akiropoka ATAJIJUU....

Mgeni wangu wa pili alikuwa uyu nilienae pichani, ni winga HATARI wa zamani nchini aliyewika haswa katika Timu ya YANGA na TAIFA STARZ aitwae EDIBILY JONAS LUNYAMILA! Kwa wale wapenda soka popote mlipo mtakuwa mnalikumbuka sana jina lake kutokana na mambo adimu aliyokuwa anayafanya Uwanjani enzi zake na kwangu mimi mpaka sasa hajatokea winga Hatari kumzidi yeye mpaka sasa na wala huyo MRISHO NGASSA wenu hamfikii huyu bwana hata nusu, kama mnabisha ulizieni kwa waliobahatika kumwona LUNYAMILA akicheza au nendeni Kampala Uganda mkaona alivyoandikwa mpaka kwenye madaladala yao! Kwa wale wapenzi wangu kama kawaida subirini tena kipindi changu kesho Jumamosi saa 12 kamili jioni muone nitakuwa na wageni gani wengine....

5 comments:

Anonymous said...

wewe ndo unamfikia lunyamila si mrisho ngasa.................................c..........s.........er

Anonymous said...

we ndo unamfikia naskia umesajiliwa coventry na london unachezea mpira wa kudaiwa

Anonymous said...

Haswaaa!!!!mi nakubaliana na wewe kabisa,mm ni shabiki wa Yanga ukweli ni kuwa Lunya enzi zake alitisha!

Anonymous said...

ushauri wa bure,naomaba uwe unatuwekea mnayoengelea kwenye kipindi,kwa mfano wengine tuko mbali na hatuoni tbc1, jaribu kulifikiria hilo, kama hii ya Lunyamila mi namkumbuka saana enzi zake na ningependa kujua aliongea nn?
mdau London

Anonymous said...

Hapo umeongea benny, Edibily Lunyamila ni mchezaji bora kabisa niliyewahi kumuona na hakna ubishi kwani alitisha wakati TZ tukiwa na golden generation ya akina HUsein Masha, George Masatu, Mwameja na wengine. Ni kukosa fikra kumlinganisha na Ngassa.

Website counter