Kwakweli kipindi cha Jumamosi iliyopita kilikuwa kitamu sana na hata wageni wangu mniliowaalika nao waliperform vizuri sana na kwenye maswala ya Interview nilianza na RASHID MATUMLA aka 'Snake Boy' kama unavyomuona apo kwenye picha na yeye alikuwa ni mmoja kati ya wageni wangu maarufu niliwaalika Studio 'LIVE' sikuiyo...
Huyu ndie aliyekuwa Bondia Bingwa wa Dunia uzito wa kati RASHID MATUMLA 'snakeboy' ambaye nilimwaalika kwenye kipindi changu Juzi jumamosi 'live' na hapa tukiwa Backstage kabla sijamuingiza Studio, na kikubwa zaidi tulichozungumzia kwenye mahojiano yetu ni suala la yeye kutengua uamuzi wake wa kustaafu Ndondi baada ya kushauriwa na mwalimu wake wa sikunyingi Habib Kinyogoli ingawa mimi nilimwambia sikuizi kiwango chake kimeshuka kutokana na umri kusonga na vijana hodari wameshajitokeza kama vile kina Cheka na wenzake but akanijibu kwamba yeye anajiamini yuko Fit na anajiamini ingawa mapambano ya karibuni amekuwa akipigwa na vijana hao! Duuh jamaa kanichomolea kuhusu kustaafu maana mie nilimshauri ivyo ili kulinda Heshma yake kwa hao mabondia chipukizi maana wanapiga ngumi si mchezo ila ndio ivyo kanichomolea....
Mgeni wangu wa pili Studio alikuwa ni huyu kijana nilienae pichani, Mwigizaji chipukizi maarufu wa Filamu nchini YUSUPH MLELA! Na kwa kifupi tuliongea mengi ila kubwa zaidi ni ile Ishu yake wa kupigana 'live' na Mwigizaji mwenzie HEMED SULEIMAN wakati wanarekodi Filamu flani ivi, na akasema walikwaruzana kwa ishu ambayo hakuitaja live na akasema hana muda wa kujibizana na bwan mdogo uyo maana pengine anatafuta Bifu la kutaka umaarufu kupitia kwake! Mmmh jamani hawa vijana wana mambo nyiee, tuulizeni sie tunaokuwa nao karibu na kuyaona mambo yao loooh, Ujinga mtupu....
Mgeni wangu wa tatu na wa mwisho alikuwa ni Rapa na Mwimbaji nguli wa Dansi hapa Bongo RAMADHANI MASANJA aka 'Banza Stone'. Tuliongea mambo mengi pia na ishu kubwa ni kuhusu tuhuma zake kwamba amekuwa 'Teja' mbwia 'Unga' wa muda mrefu, na akajibu kwamba kwasasa ameacha tabia hiyo kabsaaa na hivi sasa amekuwa 'Banza Stone' mpya mwenye kujiheshimu na kujipenda na ndio maana hata afya yake imerudi kuwa nzuri kuliko zamani na kwamba hivisasa ameanzisha Bendi yake mpya iitwayo RUFITA MUSICA ambayo ana uhakika itakubalika haraka mara Album yao itakapotoa hewani, na jamaa HAJAOA ila ana mtoto mmoja wa kiume mwenye umri wa miaka 13 aitwae ALLY MASANJA! Una lolote la kuongeza apo?.....
No comments:
Post a Comment