Friday, September 3, 2010

BAADA YA KUONA JAHAZI LINAZAMA, ZIDANE AITWA TENA KWENYE TIMU YA UFARANSA....


Nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Ufaransa ZINEDINE ZIDANE 'ZIZOU. ameitwa tena kwenye kambi ya Timu iyo iliyoko CLAIREFONTAIN kaskazini mwa Ufaransa ili kwenda kuongeza Morali ya wachezaji wa timu hiyo ambao kwasasa wameipoteza baada kufanya vibaya kwenye Fainali zilizopita za Kombe ka Dunia nchini Africa Kusini na ukizingatia inakabiliwa na mechi dhidi ya Beralus leo hii. Zizou alitumia muda huo kukaa na wachezaji hao na kuangalia nao Mechi ya Fainali ya Kombe la Duni ya mwaka 1998 na ile ya Ulaya ya mwaka 2000 ambazo Ufaransa ilinyakuwa vikombe ivyo na kisha kuwapa moyo kwamba pamoja na kuwa kuna wachezaji wengi kwenye timu iyo kwasasa ila wanaweza kufanya maajabu pia kama enzi zao walivyofanya! Sasa tujiulize apa Bongo vipi mbona kina ZAMOYONI MOGELLA, JUMA MGUNDA, ABEID MZIBA SUNDAY MANARA, YASIN NAPILI, MAKUMBI JUMA, JUMA PONDAMALI, EDIBIL LUNYAMILA na wengineo mbona hawaitwi kwenye kambi ya timu ya Taifa ili kutoa 'Tips' ya jinsi gani walivyoweza kutandaza soka uwanjani kwenye nafasi zao ili madogo wa Taifa starz nao wapevuke jamani? Ukiuliza kwani hawaonekani wanasema TFF wanashindwa hata kuwapa vitambulisho vya kuingilia uwanjani kuona mechi uwanja wa Taifa, sembuse kwenda kwenye kambi ya Taifa Starz duuh AIBU kishenzi...

No comments:

Website counter