Hawa ndio wanasoka waliweka rekodi ya kuwatia Hasira mashabiki wa soka na kuwakera watu wengi zaidi Duniani mpaka sasa kutokana na kutumia mikono yao kuharibu matokeo halisi ya mechi kwa timu zao za Taifa! Kushoto ni DIEGO MARADONA wa ARGENTINA aliyetumia mkono wake wa kulia kufunga goli la mkono wakati wa mechi kati ya Argentina na England mwaka 1986 aliloliita 'goli la mkono wa mungu' na mpaka leo Waingereza hawataki kumsamee kwa kauli yakle iyo!Katikati ni THIERRY HENRY wa UFARANSA aliyeukamata mpira uliokuwa unatoka nje kwa mkono wake wa kushoto na kutoa pasi ya goli lililoinyima IRELAND kucheza World Cup mwaka huu! Kulia ni LUIS SUAREZ wa URUGUAY aliyeizuia GHANA kuingia nusu Fainali ya Kombe la Dunia kwa kuzuia kwa mikono yake 2 mpira uliokuwa unaenda kutinga wavuni na kuwaudhi mamioni ya waafrica ulimwenguni kote looh!
No comments:
Post a Comment