Thursday, July 15, 2010

SUMATRA 'YAWAFANYIA' KWELI WENYE MABASI YA ABIRIA UBUNGO...


Ile tabia ya wenye mabasi ya kusafirisha abiria mikoani kupandisha nauli zao kiholela, jana iliwatokea puani baada ya SUMATRA kwa kushirikiana na Kampuni ya Udalali nchini ya MAJEMBE AUCTION kufanya msako wa kimyakimya wa kuyakata mabasi yoote yaliyopandisha nauli kwa abiria kiholela pale UBUNGO STAND! Kwangu mie naona kama vile hawa Majembe wamewahi sana kwenda pale Ubungo, walaah wangesubiri mpaka mwezi wa 12 kuelekea sikukuu alafu maafisa wake wangetia timu pale Ubungo Stand na kujifanya abiria na haswa huu upande wa kwenda Moshi na Arusha ndio watashangaa izo nauli watakazotajiwa, wenyewe wangejiuliza kama hiyo ni nauli ya NDEGE au BASI...

No comments:

Website counter