Friday, July 2, 2010

SHIME JAMANI MKASAJILI NAMBA ZENU...


Yaani sisi wabongo bwana tunapenda sana mambo ya zimamoto! yaani hili swala la kusajili namba za simu tumeambiwa siku nyingi lakini nashangaa siku ya mwisho juzi ndio kila mtu kaenda kusajili namba yake na matokeo yake vituo vya kusajilia vikawa vimejaa hatarii, sasa sikuzote mlikuwa wapi jamani? Haya sasa serikali kwa kuwaheshimu sana imeamua kuwaongezea tena muda wa kusajili izo line zenu za simu mpaka tarehe 15 july, sasa ninavyojua mimi kuna mijitu mpaka ikifika tarehe iyo itakuwa haijaenda kwa kujifanya iko busy, sasa ngoja line zenu zikatwe ndio mtatia akili...

1 comment:

Anonymous said...

NI kweli Ben hata mm nawashangaa sana watanzania wenzangu siku za mwisho watu haooooo sijui walikuwa wapi siku zote tujitadi jamani serikali ikisema kitu tufanye muda muafaka na sio kiiiivyo, inabore, ss angalia muda huu ulioongezwa hakuna watu kwenye vibanda inamaana watu wamemaliza kusajili au ndy mnasubir ifike tarehe 15 ndy mwende?

Website counter