Friday, July 23, 2010

MJASIRIAMALI WETU LEO HII....


Yaap ni kijana wa Kitanzania aitwae aitwae JUMA SAID mkazi wa Vingunguti ambaye amejiajiri katika kazi ya kutengeneza majiko ya mkaa na kuyasambaza jijini. Kwa kauli yake anasema kwamba huwa kwa mwezi anapataga 'Oda' ya kutengeneza Majiko 400 mpaka 500 kutegemea na hali ya Biashara kwa wakati huo, na anaongeza kwa kusema kwamba kwa oda izo anazopata akitoa gharama zake zote za kununulia Malighafi ya kutengeneza majiko hayo yakiwemo mabati chakavu, hua anapata faida ya sh laki 300 mpaka 350 kwa mwezi kutegemea na upepo wa Biashara kwa mwezi husika, na kwake pesa izo zinamtosha kusukuma vizuri maisha yake! sasa kwa pesa iyo si anawapita hata baadhi ya wafanyakazi wa maofisini jamani? Je ni wangapi wanaweza kuiga mfano wa Kijana mwenzetu huyu? maana kuna vijana pale maeneo ya POSTA haswa kuzunguka SALAMANDER nawajua na wengine washkaji zangu, ukiwaona wameulamba na kupiga mavazi ya Bei mbaya ila mfukoni hawana hata Buku 2, ule mie nauita 'ujanja wa kijinga'...

No comments:

Website counter