Friday, July 16, 2010

BURIANI PROF MWAIKUSA...


Hakika utakumbuka na wengi na hasa Familia yako uliyoiacha ghafla bila kutegemea na aina ya kifo ulichokumbana nacho! Wewe ni mwanazuoni mkubwa uliyefundisha wengi pale chuo kikuu Mlimani na hata wadau wenzio wa sheria watakukumbuka sana kwa umahiri wako! Rafiki yangu aitwae SWETU FUNDIKIRA nae aliuawa na wanajeshi bila hatia kwa mtindo huohuo, sasa najiuliza kwanini Bongo hamna 'GUARANTEE' ya maisha jamani? Yaani m2 akikuchukia 2 kwa wivu wake basi ana uwezo wa kukufanya chochote atakacho tena bila wasiwasi wala kuogopa? Sasa tusubiri tuone hao waliofanya ukatili wa huu kama watakamatwa au laah na hapo ndio tutajua Jeshi letu la Polisi lina nguvu na ujanja kiasi gani kudhibiti matukio kama hayo, iyo ni TANZANIA bwana na msiifananishe na RWANDA au SOMALIA alaaah...

No comments:

Website counter