Tuesday, July 6, 2010

BARUA YA WAZI KWA 'MCHAWI' MARADONA...


Mimi BEN kama mdau wa soka nakukubali sana kwa uwezo wako wa kulipiga JABULANI uliokuwa nao uwanjani enzi zako na kwangu mimi hakuna wa kukufananisha nae mpaka sasaivi maana kwa muono wangu hata PELE hakuingii ndio maana FIFA kwa aibu wakajifanya kuwapa tuzo wote wewe na Pele lakini ilikuwa upewe wewe ! Lakini ndugu yangu wewe kipaji cha Ukocha hukuwa nacho, basi 2 kwakua ulichezaga 'Jabulani' zamani basi ukajua utaweza 2, hapo ukabugi step kiongozi looh! Ulipokuwa South kwenye mashindano uliomba utengenezewe choo cha Bei mbaya chumbani kwako, ukatengenezewa! Ukawaahidi wananchi wa ARGENTINA kwamba unaenda kulitwaa Kombe then ukirudi 2 pale mjini utatembea uchi wakakutazama 2! Matokeo yake jana umerudi kimya kimya na hata kwenye dirisha la basi pale mbele unapokaaga hukutaka kuchungulia nje kwa wale watu uliowaahidi mwanzoni, kwasababu ya mayai 'viza' yaliokuwa yanakusubiri! Na mpaka sasa huna la kusema maana ulikuwa na Timu nzuri iliyokuwa na wachezaji wakubwa duniani kibaoo! Duuh pole sanaa ndugu nyangu ila angalia usirudi kuwa Teja bwana...

No comments:

Website counter