Saturday, September 10, 2011

HAYA NDI MAMBO KADHAA USIYOYAFAHAMU KUHUSU 'KOFFIE OLOMIDE', YASOME CHINI APO...


Anaitwa kwa jina Halisi la CHRISTOPH AGBEPA MUMBA ANTOINE aka tumezoea kumwita KOFFIE OLOMIDE, mzaliwa wa Kisangani kule Congo ya DRC mnamo Tar Aug 17 1956. Na hapa leo nakuletea mambo kadhaa usiyoyajua kuhusu Koffie.

Koffie amezaliwa kwa Baba mkongo na Mama yake ni raia wa Sierra Leone! Jamaa Hobbie yake ni kuendesha Magari tangu utotoni na aliwaza kuwa mwendesha magari ya Mashindano ila akakutana na ukali wa Babake aliyemwambia 'KITABU' kwanza magari baadae! Koffie ana majina mengi sanaa ya Utani ila kwa leo ntakutajia machache tu kama vile LE GRAND MOPAO, LE SHAKE SPEAR DU ZAIRE, NKOLO LUPEMBA, GRANIBANE MAJI, KADRA KORAMAN na mengineyo mengi tu!

Baba yake mzazi ni mgonjwa kwasasa na anaishi aris Ufaransa wkt Mamam yake ni Dalali wa Madini kule Kisangani mjini. Koffie ana kaka yake mkubwa kuzaliwa aitwae JONNY KO na huwa anamtajaga sana kwenye Nyimbo zake! Jamaa ameoa na ana watoto saba mpaka sasa waitwao, ARISTOTE, ELVIS, MINOU MISS UNIVERSE, DIDIE STONE NIKE, ROCK, DEL PIERO MOURIHNO na SAIT JAMES ROLLS!

Ukitaka kumwalika Koffie kimuziki basi ujue Hotel atakayolala yeye basi na wacheza Shoo wake wa kike nao watalala hiyi hiyo ya bei mbaya, na hilo nimeshalishuhudia kwa macho yangu alipokuja Bongo kwa mara mwisho kutumbuiza maana anawachunga sanaa mabinti hao ingawa inasemekana alishatembea na baadhi yao ingawa 'SKENDO' kubwa iliyoko sasa ni tuhuma kwamba 'anatembea' huyo mwimbaji wake hapo juu kwenye picha aitwae CINDY na kuibua ugomvi mkubwa kwa mkewe alie juu pichani kutishia kuomba 'TALAKA' baada ya kusikia Binti huyo ana Mimba ya Koffie!

2 comments:

Hadj le jbnique said...

UHUSIANO WA KOFFI NA CINDY LE COEUR MBONA SIO SIRI TENA KAKA,UKO WAZI NA KOFFI KISHAMTOLEA MAHALI BI MDOGO,TEMBELEA SPORTSTAREHE.WORDPRESS.COM,Wana habari nzuri sana za hawa bana congo.Tazama hapa chini koffi akimzawadia baba yake CINDY gari la kifahari aina ya Jaguar

http://www.youtube.com/watch?v=dFX775Qx2ik&feature=related

Hapa Koffi na cindy wake wakimuimbia mamaa Edita omar bongo a.k.a.edita sassou nguesso,edita mwana ya sassaou ambae alikua ni first lady wa gabon yani mke wa rais omar bongo wa huko,na pia alikua ni binti wa kumzaa wa rais denis sassou ngueso wa congo brazaa,huyu mama alikua kipenzi cha wanamuziki,huu wimbo ni wa maombolezo kufuatia kifo chake,i luv the song binafsi
http://www.youtube.com/watch?v=Sz-2SYN_GXY&feature=related

Hapa bana QL Waliiteka Airport ya Paris kwa muda,mcheck koffi na cindy watakavoondoka hapo airport in style

http://www.youtube.com/watch?v=Wo2vRdMoKzI&feature=related

mpita njia said...

mbona umezibana hizo link alizoweka huyo mwana congo hapo juu we ben kinyaiya?sasa tutatazamaje hizo video tuone koffi akimzawadia hiyo gari babake cindy,isije kuwa ni uzushi jazz band,fanya mpango uzifungue tuzione au ziweke hadharani bloguni tutiririke nazo,nimetembelea hiyo blog sport starehe,kweli inatisha kwa habari za wanamuziki wa zaire..lakini za wabongo hamna sasa sijui inaendeshwa na wacongo ama vipi,ila kweli wako well informed pande hizo

Website counter