Wednesday, August 24, 2011

NAAMUA KUMWAGA 'MBOFUMBOFU' LEO...
Kama kuna ishu simaindi kuidiskasi wiki hii ni ishu ya futbolu, hizi mechi za hisani hizi mwanangu zinazingua nazo samtaimz...
Ujue niliwahi kuziinjoi enewei Manchesta ilipoigonga Site na kunyakua, si unajua babaako, Man U damu, juzi kati mwanangu Simba si wakataka sifa?

...mbili mwanangu, mji haukaliki kudadadeki!
Tuachane na bolu, twende sasa, mwanangu ishu ya BigBlaza naskia imepigwa nanii, au nimesikia vibaya? Naskia mtu mzima minista kachonga kweli kuhusiana na ishu ile akashauti kwamba haimsaidii chochote yanki wa kibongo.
We umemuelewa mwanangu?

..eti mwanangu umemuelewa mshua?
Manake kachongaaa, dizaini atakuwa kamaindi masista wale walivyokuwa wanachapwa na yule mchizi mmoja mara wameingia kwenye kidimbwi kile wameliwa nanii, watu wanashangilia, na kama unakumbuka kipindi kile mtu mzima Gaetano alivyokuwa anamzingua yule mtoto wa kisauzi, ..unakumbuka?

Unaambiwa kuanzia pale ndio kipindi kikapata maileji, kila mtu unaambiwa akanunua dishi nini, ..biznes inafanyika na watu wakawa wanachukulia poa tu sijui sasa kipindi kile kulikuwa hamna viongozi wanaoangalia maadili au dizaini walikuwa wamepozwa kimtindo, mimi hata sijui ninachokumbuka ni Bata tu maana tulikuwa tunajimiksi kweli na masupastaa wetu akina Mwisho, Richard ndio alikuja na mkwanja na wengineo.

Wengineo siwataji maana walikuwa mademu na si mnajua masista walivyokwenda kuzingua? Hwajazingua sana lakini mbona akina mwisho na Richard nao walinanii watoto wa watu bwana?

Hamkuona kipindi kile kwamba ilikuwa nje ya maadili washua?
Sasa mwanangu mkuki mara nyingi unakuwa fresh kwa kitimoto lakini ukija kwa hyuman biing inakuwaga noma sana, unauma, na ninahisi ndio sababu mshua kamaindi kitaa, na kisha kaendelea kwenda kumaindi mjengoni kwamba ishu haisaidii chochote jamii ya mayanki.

Dizaini mshua kimemchoma mabinti wale kwenda kuchezewa huku sisi tunaona kisha mwisho wa siku mtu kama Bhoke hatumuoni tena kwenye kioo, sijui jamaa wamemtema?
Umeona?

Kawa supastaa sawa, lakini kadhalilika ingawa mwenyewe anadai hajutii, na kazi dizaini sijui kapumzika au kapoteza, na alichopata sana sana ni nini.

Ukiuliza kaenda kufanya nini kule atakujibu nini?
Hihihihihihi...
Na ule mkwara wa mjengoni usikute ndio unaishia pale, yaani hamna tena kitakachofuata?

washua wetu hawa wanachoooonga wakiwa mjengoni lakini wakija kitaa wanatulia, kama sio kutulizwa, sasa nahisi kunanhaja ya kuwashtua kwa hedlaini kama hiyo hapo juu au sio mwanangu?

Ndo' manake si ndio?
Eksheni wazee acheni kuchonga sana kuna haja ta kutenda kudadadeki!
Tchao...

1 comment:

Anonymous said...

Mwanagu kinya Vp bata Hapo kwa Malkia? mwanangu umelonga kweli hiyo ishu mwanangu hata mimi imenigusa sana sana hawa washua huwa wanawaza nini ktk vichwa vyao hawana ishu za maana za kudiskasi na kuchangia mjengoni au? nakosa neno zuri la kulonga!!!!!!!!!!!!,hivi tunakwenda wapi na hawa washua wetu mjengoni?

Website counter