Saturday, August 20, 2011

HAYA NDIO MAAJABU YA PAKA MLA MAJANI...


Ukistaajabu ya Musa basi umeliwaaa! Amini usiamini weekend iliyopita nilialikwa Nyama Choma katika mji wa MILTON KEYNES ambao uko umbali wa mwendo wa lisaa limoja kwa gari kutoka hapa South London nilipo sasaivi, sasa uwani kwenye hiyo nyumba ya 'SHUGHULI' kulikuwa na 'PAKA' mmoja ambaye alinishangaza sana kwakweli na ndio ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuona tukio hilo maishani mwangu! Ebwana Paka huyu alikuwa anakula majani kwa 'FUJO' kama Mbuzi vile! We fikiria sie tulikuwa tunachoma nyama lakini wala yeye hakuwa na habari ya kuja kutudoea nyama kama walivyo Paka wengine Duniani ila yeye alikuwa anafakamia majani 2, na ndio maana nikamua japo kwa picha hizi nanyi mushuhudie hili nisemalo kwakweli looh, ni MAAJABU HAYAA...

Yaani ni mwendo wa kula majani kama Mbuzi vile...

2 comments:

Anonymous said...

huyo paka atakuwa vegeterian

Anonymous said...

Kakosa nyama na panja inabidi kula majani.

Website counter