Saturday, July 23, 2011

ZIARA YANGU YA KWA WAZIRI MKUU DODOMA ILIVYOKUWA KWA UFUPI...

Hivi karibuni tena mimi na baadhi ya wasaani tulifanya ziara ya kwenda Dodoma kwa mualiko wa Waziri mkuu wetu Mh MIZENGO PINDA. Ziara yetu ilikuwa nzuri sana na Waziri mkuu alitupokea vizuri na kutukirimu vizuri kwa muda wote wa siku 3 tulizokuwa uko...

Pia tulikaribishwa ndani ya Bunge na kupewa nafasi ya kujitambulisha mmoja mmoja kwa waheshimiwa Wabunge nakwakweli walitufurahia sanaaa maana wengine wanatusikiaga tu ila sikuhiyo tukaonana 'LIVE', kwa hakika ilikuwa raha saanaaaa! Pembeni yangu Wasanii RAY KIGOSI na STEVE NYERERE.

Pia tulipata nafasi ya kukutana na baadhi ya Mawaziri na wabunge ambao pia ni rafiki zetu wa karibu na kubadilishana nao mawazo, kwenye picha baada ya mimi ni Mbunge mzee NIMROD NKONO na waziri wa vijana na Michezo Mh EMANUEL NCHIMBI...

Huyu pembeni yangu ni waziri wa Viwanda Mh CYRLY CHAMI ambae alinishangaza sana baada ya kuniambia anamjua saana Baba yangu mzazi Mzee KINYAIYA na kwamba wanatoka wote kijiji kimoja looh, nikabaki kucheka tu na kupewa kazi ya kufikisha salamu kwa mzee...

Huyu Waziri mkuu wetu bwana, cha kushangaza wakati naongea nae kwanini asianze kunipa story za shamba lake la Nyuki na Asali na mambo ya Kilimo uko kwao! Mzee anapenda sana Kilimo huyo looh...

No comments:

Website counter