Wednesday, July 27, 2011

KWENYE KONA YA MAHABA LEO HII...


NAAM wapenzi wa kona yetu ya Mapenzi na Uhusiano inayozidi kujiongezea wasomaji kila kukicha kutokana na watu kuguswa na mada. Hali hiyo inanifanya kichwa changu kichemke ili kuhakikisha kila ujumbe ninaotoa kwa wasomaji uwe na faida kubwa zaidi.

Leo nina swali moja kati ya maswali ambayo yanafanana kwa njia moja au nyingine, nalo linasema hivi linasema hivi:“Nina mpenzi wangu ambaye tuna mwaka sasa tangu tuanze uhusiano wetu, hatujaoana wala kupata mtoto, lakini tatizo la mpenzi wangu tunapokosana ana nuna na hata kukataa kuongea na mimi.“Kuna wakati ninapompigia simu hukata, tabia hii inanisumbua sana na kuninyima raha hata kama nina kuwa nimemkosea unakuta nashindwa kuelewa tatizo langu ili nijirekebishe.“Mpenzi wangu nina mpenda na kumuacha siwezi lakini tabia zake huninyima raha naomba msaada wako, nifanyeje?”Kwanza napenda kuwapeni pole wote mliokumbwa na maswahibu kama ya aina hiyo, ni kweli mpenzi wako anapokaa kimya anakuchanganya mara mbili na kuwaza hata visivyo wazika.Japo ni kweli kuna jambo limemkwaza lakini kukaa kimya si utatuzi wa tatizo, isipokuwa ukifanya hivyo unazidi kuumia zaidi ya alivyoumia.Siku zote mwenye tatizo huumia kwa kujua tatizo lake, lakini asiyejua huchanganyikiwa na kujikuta akichanganyikiwa mara mbili.NINI CHA KUFANYA?Siku zote wanadamu tumeumbwa tuna upungufu mkubwa na dawa yake ni kukumbushana au kukosoana ili turudishane kwenye mstari. Siyo kwamba umejua unapendwa basi kosa si kosa, unanuna hata hutaki kuzungumza na mpenzi wako.Amechelewa kidogo basi hutaki kuongea naye au akipiga simu unamkatia, Hayo si mapenzi, mapenzi ya mtindo huu huyaita ya mateso na ya upande mmoja. Penzi la kweli haliumizi bali lina huruma na lina maonyo.Hata kama mpenzi wako amekuudhi mueleze tatizo lake si kukaa kimya au kukataa kuongea naye hata kumkatia simu.

Jiulize unachomfanyia mwenzio ukifanyiwa utafurahi? Hii yote hutokana na ulimbukeni wa mapenzi kwa kujua unapendwa basi unafanya upendavyo hata kama linamuudhi mwenzio.Muonee huruma mwenzio akuonyeshapo upendo na wewe muonyeshe, si wajinga wasemao upendwapo pendeka, utakuja penda pasipo na penzi na kujuta wakati huo itakuwa ‘too late’ (umechelewa).Mwisho jiulize wazuri kama wewe au hata kukuzidi huwaoni wanavyo tafuta penzi la kweli, lakini wanaishia kukutana na wanaume baa na kuachana kwenye nyumba za wageni na kudodea nyumbani.Penzi la mateso na karaha za kila siku linapunguza upendo moyoni. Itumie nafasi hii adimu kuyajenga maisha yako mapya yenye furaha ya pande mbili. Ni makosa kutumia kosa la mwenzako kama bakora ya kumpigia.

No comments:

Website counter