Thursday, July 28, 2011

KUMBE UHUSIANO WA GENEVIVE NA D"BANJ NI "FAKE", IMEGUNDULIKA...

Mwanamuziki DBANJ akiwa na Bi. FLORENCE kwenye siku ya kusheherekea kutimiza miaka 64 ya mwanamama huyo "mpenda Serengeti Boyzz"...

UHUSIANO wa kimapenzi kati ya mwanamuziki, D’Banji na muigizaji Genevieve Nnaji wote wa Nigeria, si wa kweli na upo ili kuficha mapenzi ya siri kati ya D’Banji na mwana mama maarufu ambaye ni Mwanasiasa Tajiri Bi. Florence Ita Giwa.

Habari zinasema uhusiano wa kweli uliopo ni kati ya D’ Banji na Florence, ambaye ni mwanasiasa mashuhuri nchini humo.


Kwa mujibu wa taarifa za jarida moja la mtandaoni nchini Nigeria, Florence anasifika kwa kuwa na mahusiano na vijana wadogo na kuwagharamia kila kitu.Habari zaidi zinasema D’Banji alipendekeza kwa Florence wawe na uhusiano wa siri na mwanasiasa huyo alikubaliana na pendekezo hilo.

Hivyo ili kuendelea kuficha ukweli huo, D’Banji alianzisha uhusiano huo Genevieve ambao ni wa kikazi zaidi, na kuukuza ili kuficha kilicho nyuma ya pazia.

No comments:

Website counter