Thursday, July 28, 2011

JAMANI RAFIKI ZANGU HAWA WAMEGOMBANA TENA JAMANI...UHUSIANO kati ya wasanii nguli nchini Uganda, Bebe Cool na Jose Chameleon unazidi kudorora baada ya wasinii hao wiki hii kufanyiana vituko vinavyoashiria kuwa na ‘beef’ la chini kwa chini kati yao.


Kwa mujibu wa mtandao wa jarida la Redpepper la Uganda, uhusiano wa wasanii hao ulianza kuzorota baada ya Chameleon kutoswa dili la kufanya maonyesho yake katika klabu ya usiku ya Monalisa ambapo awali alikuwa na ratiba ya kufanya maonyesho yake kila Alhamisi.


Taarifa zaidi zinadai kuwa Chameleon alikuwa akiingiza karibu Sh milioni tano, fedha za Uganda kila mwezi, ambapo hivi sasa uongozi wa klabu hiyo umeamua kumpa dili hilo Bebe Cool ambapo inasemekana Chameleon anaamini kuwa Bebe Cool amemzunguka na kupewa dili hilo.

No comments:

Website counter