Sunday, June 5, 2011


Huyu apa kushoto anaitwa MAJALIWA ambaye ni mwanamuziki pekee nchini mwenye uwezo mkubwa wa kuiga na kuimba 'VIPANDE' vyooote alivyokuwa anaimba 'NGULI wa Muziki' marehemu TX MOSHI pale Msondo Ngoma na kama huamini nenda wanakopiga Msondo alafu kaa 'Getini' alafu sikiliza sauti ndani, utadhani TX MOSHI yupo stejini daah...

Huyu sasa ni Mtoto wa kiume wa aliyekuwa Mwanamuziki 'NGULI' nchini marehemu TX MOSHI aitwae TX JUNIOR ambaye kwasasa pia ni mwanamuziki wa Msondo akiwa napikwa vyema kuja kuziba vizuri pengo la babake ambaye pia ana 'HISA' ndani ya Bendi hiyo Kongwe yenye maskani yake ILALA jijini Dar...


Basi bwana Msondo pia wana wacheza 'SHOO' wawili 'MATATA' sanaaa kunako kuyumbisha 'NYONGA', na huyo dada apo kulia 'Mkongwe' MAMA NZAWISA, yaani anakata kiuno ka FENI vile duuh...

No comments:

Website counter