Sunday, June 5, 2011

ZIARA YANGU KWA WANA 'MSONDO NGOMA' LEO ILIVYOKUWA...


Leo Jumamosi hii usiku huu niliwatembelea wana 'Baba ya Muziki' Wakongwe MSONDO NGOMA pale kwenye Bonanza lao la kila Jumamosi jioni ndani ya viwanja vya TCC chang'ombe jijini Dar kupata burudani ya 'KALE' kidogo! Sasa kwa taarifa yako ni kwamba Bendi ya Msondo ina waasisi 2 waliobaki hai mpaka sasa baada ya Marehemu TX MOSHI kutangulia mbele ya haki, akabaki mzee MAALIM GURUMO na chuma kingine apo juu pichani mkongwe SAIDI MABERA! Na baada ya mzee GURUMO kuanza kuumwa basi jahazi la MSONDO analiongoza 'Gwiji' huyu ambaye ni mcharaza 'GITARE' hatari nchini mzee MABERA, na kwa hakika ilikuwa ni burudani safi sana kwa watu kama sie tunaojua muziki halisi uko wapi tehee etee teheee...

Huyu ni ROMAN MNG'ANDE aka 'ROMARIO', ni rapa na mpuliza 'TRUMPHET' mahiri nchini, ni kiraka kila sehemu na mpaka DRUM pia anapiga! ni rafiki yangu mkubwa kuliko wanamuziki wooote wa MSONDO NGOMA waliopo sasa, ni mtu mchangamfu sanaaa...

No comments:

Website counter