Monday, June 13, 2011

HII NI 'REKODI' MPYA SASAIVI DUNIANI....


Huyu bwana anaitwa JUNRAY BARAWING kutoka UFILIPINO ambaye jana alitawazwa na wataalamu wa kile kitabu cha kuweka kumbukumbu za maajabu Duniani cha 'GUINNESS' kwamba kwasasa ndie mtu mfupi kuliko watu wooote wanaoishi Duniani kwasasa akiwa na urefu wa inchi 23 yaani cm 58 akiwa amepungua inchi 3 zaidi ya alikuwa akishikilia Record hiyo KAGHENDRA MAGAR kutoka Nepal! JUNRAY ametimiza miaka 18 juzi na kumfanya atambulike kama mtu mzima kwa sasa na ndipo Chief Editor wa 'GUINNESS' bwana CRAIG GRENDAY alipolazimika kutumia masaa 24 kumpima JUNRAY ili kujua kimo chake kamili kabla ya kumtawaza 'RASMI' kama mtu mfupi kuliko wooote Duniani alie hai kwasasa...
Website counter