Friday, May 20, 2011

TIMU YA 'BONGO MOVIE CLUB' KUONDOKA KESHO JUMAMOSI KWENDA MWANZA KUTOA 'DOZI' KAMA KAWA...


Hiki ni kikosi kizima cha 'MAUAJI' cha BONGO MOVIE CLUB ambacho kesho JUMAMOSI kinaondoka DAR na kutua katika Uwanja wa 'NDEGE' wa Mwanza majira ya mchana kwa ajili ya kucheza mchezo wa kirafiki wa 'KIMATAIFA' na Timu ya 'MWANZA MEDIA ALL STARZ' amb ayo ni timu ya mjumuisho wa maDJ na watangazaji wa MWANZA katika pambano kali la SOKA litakalofanyika katika Uwanja wa CCM KIRUMBA mjini Mwanza keshokutwa JUMAPILI saa 10 jioni. Kikosi kitakachoondoka kesho kitajumuisha NYOTA woote kama vile BEN KINYAIYA, MASANJA MKANDAMIZAJI, RAY, KANUMBA, JB, CLOUD, RICHIE RICHIE, HATMAN MBILINYI, STEVE NYERERE, JIMMY MASTER, TINO, SHIJA, RADO, CHIKI, CHECBUDY na wengineo! Kwa MADEMU watakaoandamana kusafiri kesho na kikosi ni WEMA SEPETU, ODAMA, JAQ WOLPER, SHILOLE, MAINDA, JAQ PENTEZEL, ROSE NDAUKA, KATE wa mambo hayo, SNURA na wengineo! Kwaiyo wakazi wa kanda ya Ziwa ni fursa yenu kuja kujazana ndani ya uwanja wa CCM KIRUMBA keshokutwa Jumapili kuwashuhudia 'NYOTA' wenu wa 'FILAMU' nchini wakitoa 'DOZI' kwa maDJ na Watangazaji hao wa MWANZA!

Haya ni mazoezi yetu ya mwisho tuliyofanya leo kwenye uwanja wa LEADERZ CLUB Kinondoni jijini Dar tayari kabisa kwa 'MTANANGE' huo wa keshokutwa Jumapili jijini MWANZA!

Hapana 'CHEZEA' mimi weyee, lazma niwatungue iyo Jumapili kudaadekiiii...

Nikiwa na MASOUD BITEBO, ambaye ni mtoto wa nyota wa soka wa zamani nchini KHALID BITEBO aka ZEBWELA! Nyie subirini MAVITUZZ yetu keshokutwa pale kati 'CCM KIRUMBA' jumapili...

Huyu ni 'STRAIKA' wetu wa Maana na sikuhizi RAY amekuwa 'FIT' sanaaa, usidanganyike na icho kitumbo apo weeee anakimbiza huyooo, subirini mtamsikia keshokutwa Jumapili akiunguruma CCM KIRUMBA...

No comments:

Website counter