Monday, May 9, 2011


Nikiwa na rafiki zangu, kuanzia kulia ni Kamanda wa POLISI wa zamani wa moa wa Mwanza Bw. JAMAL RWAMBO, anayefuata ni winga machachari MRISHO NGASSA na mkewe kushoto ni Nahodha wa Timu ya soka ya Taifa SHADRAQ NSAJIGWA aka 'Fuso' ambaye alitwaa Tuzo ya mwanamichezo Bora wa Soka wa TASWA...

Wakati wa 'Msosi' nikambamba Bondia maarufu nchini RASHID 'snake boy' MATUMLA, akiwa na Baba yake mzazi Mzee MATUMLA pembeni yake na nyuma ni mdogo wake ambaye pia ni Bondia MBWANA MATUMLA...

Huyo apo kushoto ndie Mwanasoka bora wa kike nchini, anaitwa ASHA RASHID aka 'Mwalala' na hapa anaonyesha Tuzo yake aliyoitwaa juzi usiku! Huyu demu aliwapoteza sana watu juzi maana alipoingia ukumbini hakuna aliyemjua kutokana na jinsi alivyojiremba na alivyovaa tofauti na sikuzote anapoyapigilia 'MAJEANS' yake na flana ila alipoitwa kwenda kupokea Tuzo yake ndio watu nao wakabaki kushangaa na wengine kuangalia 'VIGIMBI' vyake miguuni na kubaki kusema "Haaa hii nayo Video"...

Nahodha wa Taifa Starz SHADRAQ NSAJIGWA wakati akitoka jukwaani kupokea Tuzo yake...

No comments:

Website counter