Tuesday, April 5, 2011


Yaap nilitua kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza majira ya saa 1 usiku ivi na moja kwa moja nikaelekea Hotelini tayari kusubiri 'pakuche' ili nikafanye kazi iliyonipeleka kule jijini Mwanza...

Baada ya kumalika 'KAZI' yangu iliyonipeleka, nikaenda kufanya Interview kwenye Radio ya Passion FM na wasanii maarufu wa Bongo Flava waliokuwepo mjini Mwanza kwa ajili ya kucheza mechi ya Hisani na watangazaji na Madj maarufu wa Mwanza ilifanyika Uwanja wa CCM KIRUMBA na mie pia nikaalikwa kucheza mechi hiyo ili kuihamasisha zaidi, kwenye picha kuanzia kushoto ni H.BABA, INSPECTOR HARUNI, JEBY na SUMA G...

Muda wa mechi ulipowadia tukajitoma ndani ya ya Uwanja wa CCM KIRUMBA pamoja na wana Bongo Flava woote unaowajua...

Niliongoza safu ya ushambuliaji ya BONGO FLAVA FC kwa hakika niliwasumbua sana juzi na hawatanisahau ingawa matokea yalikuwa ni Droo ya bao 2-2 na magoli ya timu yetu nilifunga mimi na H. BABA! kwenye picha baada ya mimi ni SUMA G na KALA PINA...

No comments:

Website counter