Wednesday, April 6, 2011

ZIARA YANGU YA MKOANI MWANZA KWA UFUPI...


Nimegundua watu wa Mwanza wanapenda sana kujirusha na iyo hapo pichani ni Bendi maarufu jijini Mwanza iitwayo 'SUPER KAMANYORA' ambayo inatumbuiza kila weekend ndani ya ukumbi wa VILLA PARK ulio karibu na uwanja wa mpira wa CCM KIRUMBA! pichani ni waimbaji wakongwe waliowahi kutamba na Bendi mbalimbali nchini, kushoto ni RASHID MWENZINGO aliyewahi kutamba na BENDI za TAMTAM MCHINGA SOUND, TOT na nyinginezo na huyo mwanamama kulia ni ANNA MWAOLE aliwahi kutamba na SIKINDE, VIJANA JAZZ na nyinginezo, sasa wanatamba na KAMANYOLA BAND na wamelishika kwelikweli jiji la Mwanza kudaadekiii...

Nikilitaja jina BENNO VILLA nadhani wapenzi wengi wa Dansi watakuwa wanamjua mzee huyu ambaye kwasasa ndie kiongozi wa Bendi ya 'SUPER KAMANYOLA' ya jijini Mwanza! Ivi karibuni kulikuwa na minong'ono kwamba atahamia SIKINDE baada ya mwimbaji wake SHAABAN DEDE kuhamia MSONDO, ndipo uongozi wa Bendi ya Sikinde ulipohaha kumsaka mwimbaji huyu mkongwe aliyewahi kutamba na bendi za SIKINDE, VIJANA JAZZ enzi hizo za 'OGOPA MATAPELI' ambao aliutunga yeye na ukavuma saanaaaa, ni mtu mkarimu na ni rafiki yangu sana, BRAVO BENNO VILLA...

Baada ya kutoka kuwatembelea SUPER KAMANYOLA BAND ndipo likaja balaa lingine baada ya rafiki yangu ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Flava INSPECTOR HARUNI kuumia na kuchanika vibaya mkononi baada ya kuangukia Chupa ya Bia iliyokuwa imevunjika na ikabidi tumpeleke Hospital usiku huohuo akapatiwe huduma ya kwanza daah ila alivuja sana damu...

Pole sana mshhkaji maana mkono ulichimbika sana daah...

No comments:

Website counter