Thursday, April 7, 2011

NAAAM SASA NIMEANZA KUPOKEA MICHANGO YENU KWA KIJANA MWENZETU HUYU MLEMAVU...


Huyu ni kijana Godfrey mwenye umri wa miaka 28 sasa, mwenyeji wa SINGIDA aishie kwa msamaria mwema maeneo ya Upanga jijini Dar. Ni rafiki yangu sana kijana huyu ingawa ni 'MLEMAVU' wa viungo ambaye nilimtambulisha kwenu kwenye 'BLOGU' yenu hii kumuombea kwenu msaada wa hali na mali ili niweze kumnunulia 'BAISKELI' ya walemavu ya kutembelea maana kwakweli inanitia uchungu sana kila ninapomtembelea anapata taabu sana kutoka nje na kunifikia kutokana na kutembea kwa 'KUJIBURUZA' chini jamani. Sasa habari njema ni kwamba nimeshaanza kupokea michango ya wasamaria wema wenye nia nzuri na imani ya kuwasaidia wenzao ili kufanikisha jambo hilo la kumnunulia Baiskeli ya kutembelea! Jana nimepokea mchango wa mdau mmoja aitwae JACKSON MWAKATUMBULA anayefanya kazi kwenye kampuni ya simu ya 'ZANTEL' ambaye hakutaka tuweke wazi kiasi alichotoa, nami nimeliheshimu ilo! Jamani nawaombeni wadau zaidi wajitokeze zaidi ili tujichange tuweze kufanikisha jambo hilo ili kijana mwenzetu huyu nae tumrahisishie usafiri ili nae afurahie maisha! NAKARIBISHA MICHANGO YENU YA HALI NA MALI KWA CHOCHOTE ULICHONACHO, ASANTENI...

1 comment:

Anonymous said...

Benny unategemea kuchangisha kiasi gani kwa ajili ya ununuzi wa baiskeli ya huyo kijana mlemavu

Website counter