Friday, April 8, 2011

JAMANI TUMSAIDIENI KIMAWAZO MWENZETU HUYU...ANCO BEN habari.

Mimi nina matatizo na mchumba wangu. Yeye si malaya na ni mzuri ila ana kisirani, kiburi na jambo dogo tu ananuna.

Baadaye huniomba msamaha na pia anarudia makosa yake na nikihoji ananiomba nimzoee. Sasa hivi ni mwaka wa tatu tupo katika uhusiano.

Ana tabia ya uzito kunijali mimi nikiwa na shida ama kuumwa.

Huyu mpenzi wangu anapenda nivae kama bukta, miwani mikubwa kitu ambacho hata kwa risasi sivai na kinanifanya nimfikirie kama anashobokea na matozi.

Baba na mama wa huyu mpenzi wangu wametengana, dada mtu ameachika pamoja na ndugu walio wengi wa kike hawajaolewa.

Nilishawahi kuomba ushauri kwa dada yake akaniambia mdogo wake ndivyo alivyo hata akiwa kwao.

Huwa ananiambia ananipenda sana ila nimvumilie ataacha tabia hizo, lakini huu ni mwaka wa tatu sasa yupo hivi.

Sisi tupo chuo mwaka wa pili na mimi sidhani kama atabadilika. Hataki tuachane.

Nifanyeje kaka kwani nampenda na yeye ananipenda sana ila nimechoka na ninahitaji upendo.

Paul, Dar es Salaam, 0755 681 602 au

Danspord1@yahoo.com

No comments:

Website counter