Wednesday, April 27, 2011


Huyu ni mnenguaji matata wa EXTRA BONGO aitwae FATMA KIBOSHO akipiga 'MSAMBA' kuonesha kwamba yupo 'OFISINI' kiukweli weeweeee...

Nae kiongozi wa Wanenguaji wa Extra Bongo SUPER NYAMWELA alipagawisha vilivyo haswa alipokuwa akicheza na mwenzake SUPER DANGER ambae alihama nae 'TWANGA PEPETA'...

SHUGHULI ilikuwa 'PEVU' kwenye Shoo na mpaka Staili hizi za 'KUNG FU' zilitumika pia, chezeaa wewee...

Sasa ni wakati wa kuingia uwanjani kucheza Mechi yetu tuliyoalikwa kwenye hilo Bonanza la Maveterani wa TABATA lililofanyika kwenye viwanja vya Tabata Shule jana Jumanne mchana ndipo waandishi wa habari walituvamia kutuhoji kuhusiana na ujio wetu siku hiyo na nikiwa kama 'CAPITAAIINN' wa Timu nikamwaga 'SERA' kama kawa alaaah...

No comments:

Website counter