Wednesday, March 30, 2011

NAMUHURUMIA SANA RAFIKI YANGU IVAN KWA KUIBIWA TENAA DAAH...

Kipa Yanga aibiwa mamilioni klabuni

Kipa wa Yanga, Mserbia Ivan Knezevic
MICHAEL MOMBURI
KIPA wa Yanga, Mserbia Ivan Knezevic amefichua kuibiwa zaidi ya Sh. milioni tano na kompyuta ndogo (Laptop) chumbani kwake kwenye jengo la klabu.

Ivan alisema jana Jumanne kuwa tukio hilo lilitokea Jumamosi kati ya saa nane mchana mpaka saa 12 jioni wakati akiwa amepumzika ufukweni na habari za ndani zinadai hakufunga vizuri dirisha lake kwenye chumba hicho kilichopo gorofa ya pili kwenye makao makuu ya klabu yake.

�Nimeibiwa fedha zangu dola 4,000 (sh. milioni 5.9) na Laptop yenye thamani ya Euro 600 (sh. milioni 1.3). Ni kitendo cha fedheha, yaani hapa nilipo sina hata shilingi wala sijui nifanyeje, nimeripoti kwa uongozi na Polisi Msimbazi Jumamosi iliyopita.�

Ingawa hakupenda kuingia kwa undani kuhusiana na suala hilo kwa maelezo kuwa lipo kwenye vyombo vya dola, alidai kuwa anawahisi waliomuibia lakini atawaeleza polisi.

Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga hakupokea simu kuzungumzia suala hilo lakini msemaji wa klabu hiyo, Louis Sendeu alisema:

�Hizo taarifa tunazo lakini tusingependa kuzizungumzia kwa undani zaidi kwa vile Polisi wanaendelea na uchunguzi na tunasubiri wakamilishe kazi yao tutajua cha kufanya.�

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alipoulizwa, alijibu hakuwa na taarifa za tukio hilo kwa kuwa alikuwa nje ya ofisi.

Hiyo ni mara ya pili kwa kipa huyo kuibiwa ambapo mwaka jana alikabwa na vibaka Mtaa wa Kongo jijini Dar es Salaam majira ya jioni na kuporwa vifaa na fedha taslimu.

No comments:

Website counter