Wednesday, March 30, 2011

HONGERA MDOGO WANGU LINAH...

Linah: Nilikuwa na wasiwasi sana

Masanii aliyetwaa tuzo ya mwimbaji bora wa kike na msanii mpya anayechipukia, Linah

UNAJUA kwanini Linah alikuwa hatulii sehemu moja siku ya Tuzo za Muziki za Kili Jumamosi iliyopita? Msome hapa.

Amekiri kwamba alikosa amani kutokana na wasiwasi wakati Tuzo za Kili zikiendelea kutangazwa juzi usiku kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

Msanii huyo anayetamba na wimbo wa �Bora Nikimbie� alitwaa tuzo za Mwimbaji Bora wa Kike na Msanii Mpya Anayechipukia.

�Nilikuwa na wasiwasi sana hasa ile tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kike, nilikuwa nashindana na watu wengi wazuri ambao yeyote yule alistahili kama nilivyokuwa mimi.

�Nilijiweka tayari kwa lolote lile ndiyo maana hata nilipotangazwa nikashindwa kujizuia nikatokwa na machozi ya furaha, tuzo hizi zimenipa changamoto sana ya kujiendeleza zaidi na kuboresha kazi zangu,� alisisitiza msanii huyo.

1 comment:

muddy washington said...

ohooo!vipi tena kaka mbona habari ya picha hii haieleweki?maana umesema unamuonea tu huruma kwa kuibiwa tena!kaibiwa nini?wapi?ilikuwaje hujatuambia,blog kazi yake kupasha habari,so ukipata tetesi zifuatilie then tuletee taarifa kamili ndio itakua mzuka

Website counter