Wednesday, March 16, 2011

MAANDALIZI YA KOVA CUP YALIVYOKUWA JUZI KABLA YA MECHI YA UFUNGUZI...


Kwakweli maandalizi ya mechi hiyo iliyopigwa juzi kwenye uwanja wa Taifa jijini yalikuwa makali sana yalioendana na mazoezi makali sana katika Uwanja wa Leaderz Kinondoni na Timu yetu ya Polisi Jamii iliwakutanisha watu woote maarufu wa fani mbalimbali nchini tuliojumuika pamoja kuicheza mechi hii ya Hisana kwa ajili ya ufunguzi wa michuono ya KOVA CUP inayodhamini na kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar SULEIMAN KOVA! Hapa ni mimi na JOTI tukiwa Hoi taaban kwa kuchoka daah.....

Ila jamaa kwa 'UROHO' simuwezi loooh, yaani kilakitu anataka kula duuh...
Hapa ni H.BABA, ALLY KIBA na BEN KINYAIYA mara baada ya mazoezi...

Mwangalie anavyofanya, mwenzie napata maelekezo kutoka kwa 'TICHA', yeye anaduwalia picha looh...

Mwanamuziki wa Bongo Flava ALLY KIBA nae alikuwa hoi baada ya TIZI...

No comments:

Website counter