Tuesday, March 8, 2011

JAMANI MSONDO NGOMA BADO WANATISHAAAA...


Ama kweli 'NYOKA HAZAI PAKA' hata sikumoja, ni kweli kabsaaaa! Jana nilitembelea Bonaza la Bendi kongwe nchini ya MSONDO NGOMA ndani ya viwanja vya TCC chang'ombe aka 'baba ya muziki' na kukuta kijana huyu aitwa TX JUNIOR ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mmoja kati ya waasisi wa Msondo marehemu TX MOSHI WILLIAM! Nae ni ana kipaji kikubwa cha uimbaji kama marehemu babake na kilichoniacha HOI zaidi ni jinsi sauti yake ilivyofanana na ya Babake kwa kila kitu na ndani ya Bendi hiyo yeye ndie huwa anaimba 'VIPANDE' vyooote vya nyimbo za babake alivyoimba ndani ya Bendi hizo, na asipobweteka atafika mbali kimuziki...

Huyu ni ROMAN NGANDE aka 'Romario' ambaye wapenzi wengi wa MSONDO NGOMA wanampenda saanaaa kwa machachari yake jukwaani, na huwa ana 'rap' na kupiga 'Trumpet! Ni mtu mwenye roho nzuri sana nje ya jukwaa na ni rafiki yangu mkubwa, aaah Romariiiii....

No comments:

Website counter