Wednesday, March 23, 2011

HATIMAYE MICHAEL ESSIEN AMWOMBA RADHI BABAKE MZAZI...


Kiungo nyota mwenye nguvu kama 'NYATI' wa timu ya wazee wa Darajani CHELSEA ya England MICHAEL ESSIEN jana amempigia simu baba yake mzazi mzee JAMES ESSIEN na kumwomba radhi kutokana na Msuguano wao wa miaka mingi uliotokea! Essien ALIMSUSA babake mzazi na kukaa bila kumwona wala kumpigia simu babake mzazi kwa miaka 15 kutokana na madai kwamba babake hakumtunza alipokuwa mdogo, kitendo kilichopingwa vikali na babake aliyesema kwamba mtoto wake huyo amejazwa maneno na mamake ili asimtunze kwa lolote! 'Tatizo Michael amekulia kwa Mamake na huko ndio alikoharibika, mie niliachana na mamake miaka mingi iliyopita na mimi ndie niliyempeleka michael sekondari na kumsomesha na sisemi ivyo ili kuomba msaada kwake maana hajawahi kuninunulia Gari wala kunijengea nyumba kama anavyotangaza kwa watu, nipo tu na umasikini wangu na hapa nilipo ni mgonjwa ila najaribu kuweka wazi kwamba nilijitahidi kumuhudumia kwa uwezo wangu ingawa sikuwa na kazi' alisema mzee JAMES ESSIEN ambaye alichukizwa na kitendo cha Michael kumu 'Ignore' kwa kumfungia vioo vya gari bila kumsalimia wala kumpa 'Lift' wkt alipofunga safari kutoka kijijini kwake KUMASI mpaka Hotel ya Sheraton jini ACCRA kumwona mwanae aliporudi nchini humo kuichezea timu ya Taifa ya GHANA na kuapa kwamba kama amemdharau kiasi icho kwa kujazwa maneno na mamake basi na yeye kuanzia siku iyo Michael asitumie tena jina lake la 'ESSIEN' na aende akalitumie jina la mamake anayemwona wa maana zaidi kuliko yeye! Hapa nilipo sijamuona wala kuwasiliana nae kwa zaidi ya miaka 15 na hata namba yake ya simu sina na kila nikimwomba mamake anipe namba ya Michael ananinyima ila nashukuru jana amenipigia simu na tumeongea kwa kirefu kama baba na mwanae na ameahidi kuja kuniomba radhi uso kwa uso, ni damu yangu na bado nampenda sana ingawa watu kokote ninakoenda wananicheka kwamba mie ni masikini wakati mwanangu ni Bilionea' alisema mzee ESSIEN.

No comments:

Website counter