Thursday, March 24, 2011

DUUUH SIKIA HII...

Mume wangu amenigeuza ‘house girl’Image

KAKA BEN, mimi nimeolewa tangu mwaka 1995 na katika miaka yote hiyo nimejaliwa kupata watoto wawili, Christina na Christopher.

Mimi sifanyi kazi, ni mama wa nyumbani na mume wangu amekuwa akinitunza vizuri na watoto wangu na hanifanyii ukorofi wa aina yoyote, lakini tatizo ndani ya ndoa yetu ameshaniletea watoto wa nje watano aliowazaa tukiwa tumeshafunga ndoa.

Sasa hivi nyumbani kwangu kuna watoto saba na wiki chache zilizopita nimepata taarifa amempa ujauzito mwanamke mwingine, tena jirani yangu.

Kitendo cha kuzaa hovyo na kuleta watoto nyumbani kimeshanichosha, kwani naona sasa amenifanya ‘hausigeli’ wake.

Kati ya watoto wake hao watano, wawili ni mapacha aliwaleta nyumbani wakiwa na miezi sita na nikawalea kama wanangu hadi sasa wana miaka sita na mara kwa mara wanaumwa na mimi ndiye ninayelala nao hospitalini.

Naomba ushauri wako kwani siwezi kuvumilia tena tabia yake hii.

Mama Christina, Dar es Salaam.

4 comments:

Anonymous said...

DUH! hii habari imenistua sana, pole sana mama Christina, kabla ya yote naomba nikupe hongera kwanza kwa moyo wako wa uvumilivu uliokua nao mpaka kufikia kuletewa watoto wa nje tena 5 na ukawalea bila tatizo huyo ni moyo wa pekee kwa mwanamke yeyote wa kisasa.
Turudi kwenye mada hasa suala la ushauri,kwanza tambua kuwa hapo ulipo maisha yako yapo hatarini kwa suala la maambukizi ya maradhi hasa ukimwi, kitendo cha kuletewa watoto kila kukicha kinadhihirisha wazi jinsi mume wako anavyotembea hovyo na wanawake tena bila hata kutumia kinga yeyote kitu ambacho ni hatari sana kwa afya zenu. Pili, ningekushauri uitishe kikao cha wazee wa upande wako na wake mzungumzie suala hili kwa uwazi na mjaribu kumkanya huyo mume wako juu ya tabia yake na mwenendo mzima wa maisha yake. Tatu, mshauri mume wako muwarudishe watoto wote kwa mama zao wakawalee na mkubaliane jinsi ya kuwapelekea matunzo huko huko na si kukuletea wewe na kukuzeesha bure wakati mama zao wanaponda raha, Nne, kama nimekusoma vizuri dada yangu, umesema kuwa wewe ni mama wa nyumbani, nakushauri anza kujishughulisha kama huna elimu basi tafuta hata mtaji ufanye biashara yoyote atleast uwe busy na upate kipato chako kidogo huyo mwanaume atakuheshimu, hiyo anayofanya ni dharau ya hali ya juu kwa vile amekuona umekaa nyumbani na unamtegemea kwa kila kitu thats y anakufanyia hivyo, hayo si maisha kabisa, ipo siku atakuletea na mama wa hao watoto ukae nao ndani na usiweze kufanya chochote,
wake up my sister, jipange tafuta kitu cha kufanya onesha msimamo wako na uondoe uoga, mwambie arudishe watoto wake kwa mama zao alikuoa wewe kama mke na anatakiwa akupe nafasi yako kama mke,

Anonymous said...

mama nakupa hongera na pole kwa majaribu hongera ninayokupa nikuwa mvumilivu kwa hayo mazaiba unayofanyiwa na mumeo naomba sana uendelee kuwatunza hao watoto na kuwapenda zaidi bila kuwabagua maana hao ni malaika hawajui kitu sana sana wanajua wewe ndio mama yao wakuwazaa endelea upendo huohuo maana yoote unayofanya mazuri mungu anakuona na malipo utapata kwa muumba wetu sasa mimi nakushauri endelea kuwalea hao watoto wa mume wako kwa upondo huohuo na jaribu swala lako washirikishe wazee wakanisa kama ewew ni mkirsto na pia wazazi wa upande zote mbili wamkalishe aambiwe ya kwamba akivyokuowa alikuwa amependwezwa na wewe na alirizika na wewe ndio maana akakuweka ndani kwake kama alikuwa anaona wewe hufaai angewaowa hao anaoza nawo na istoshen sasa hivi magonjwa ni mengi akaa atulie muweze kulea hawo watoto ni hayo na usiache kusali sana mungu ainusuru ndoa yenu mumeo awezekuacha hiyo tabia yake maana kwa mungu hakuna linalo shindikana

Anonymous said...

Pole sana ndugu yangu kwa yanayokusibu.Kwanza huyo mumeo hana hata haya kwa yote aliyoyatenda kuzaa nje ya ndoa ,alafu anakuletea watoto hutunze.Kwanza mama zao wako wapi mpaka wasiwalee wenyewe.Mumeo kama anajifanya anamapenzi sana na hao watoto kwanini asitume pesaa za matumizi kwa hao baby mamas ili watunze watoto wao wenyewe.Kwanza huo ni unyanyasaji anaokufanyia kukufanya wewe ndio house girl wala sio mkewe.Kama angekujali na kukuthamini asingezoa hao watoto na kukubwagia wewe ulee.Pia kumbuka magonjwa ni mengi uwezi jua anakuletea nini wewe,kwa raha zake mwenyewe.Wasiliana na wazazi wa pande zote mzungumze kama hawezekaniki ndugu yangu funga vilago uwende kwenu,na wanao pia usimuachie mtu mwingine sababu sio rahisi mtu kuwa mngwana kama wewe kukutunzia wanao kama ulivyofanya wewe.Naamini Mungu mkubwa atakufungulia macho zaidi na kupata jibu la maana,na kuondokana na mzigo ulio nao.My dear you are too good ,cute and nice to be misstreated that way.Pls omba Mungu atakuonyesha njia ya ku solve tatizo lako.

Anonymous said...

Pole sana dada yangu kwa yaliyokufika. Kwakuwa wewe mwenyewe umeshazaa najua unajua uchungu wa mama aujuae mzazi. Lakini kwa kifupi nakushauri kama unapo pa kuegemea funga virago vyako, chukua watoto wako wawili, utokomee. Mungu ameshakuona uliyoyafanya kuwa ulikuwa na moyo mzuri wa kuwalea watoto wa huyo baba, sasa basi atakufungulia njia na mambo yako yataenda salama.

Website counter