Monday, February 28, 2011

'A TO Z' YA MECHI BAINA YETU BONGO MOVIES FC NA BONGO FLAVA FC ILIVYOKUWA....


Kambi ya Timu yetu ya 'BONGO MOVIES FC' tuliiweka ndani ya Hotel ya LAMADA pale Ilala na masaa machache kabla ya Mechi rafiki yangu MIRAJI KIKWETE ambaye ni mtoto wa Rais KIKWETE alitutembelea kambini na ili kutupa MORALI kama shabiki ingawa alipinga sana kwa sisi kuvaa jezi nyekundu kwakua Babake ni 'YANGA' damu na haipendi Jezi ya Rangi nyekundu daaah...

Nikiwa na swahiba JOTI kambini muda mchache kabla ya kwenda Uwanjani kuwavaa BONGO FLAVA FC...

Tukisikiliza mawaidha ya Kambi muda mchache kabla ya kwenda Uwanja wa Taifa, AUNT EZEKIEL nae hakukosekana banaa...
Kambi ilikamilika, na hapo kina MASANJA, MZEE ULOTU na YUSUPH MLELA wakifuatilia mawaidha yanayotolewa...

Sasa tumeshavaa JEZI tayari kuelekea uwanja wa Taifa kuwavaa Bongo Flave FC, na pichani wanaonekana wataalamu wa Benchi la UFUNDI kina MZEE CHILLO, HATMAN na BI MWENDA wakirekebisa mambo...

No comments:

Website counter