Saturday, February 5, 2011


Na wakati naenda pia nikaliona ilo 'Fuso' ambalo kuna jamaa hapo nyuma wamening'iniza Paja la mbuzi bila kujua sio vizuri kiafya, na hapo ndio natambua ni kwanini sisi 'wabongo' tunakufa mapema kiumri, ni kwasasabu hatuna HESHIMA kwenye utunzaji na ulaji wa vyakula vyetu amini usiamini...

Waangalie jamani wanatia huruma ingawa wana nyuso za matumaini ila hawajui kwamba kwa vipaji vyao walitakiwa wawe wafanyabiasha waliojitanua na kuwa na maisha mazuri kuliko 'WAZIRI' wa nchi hii ila ndio ivyo tena...

Kwakweli sikuzote heshimu mtu anaefanya kazi kwa mikono yake ya 'kibin adamu' alafu akakutolea kitu kam a hiki... Hakika ni kipaji cha hali ya juu sana ila tujiulize kwanini wachongaji hao apo juu bado wanakufa masikini wakti Ulaya kuna vijitu vinachora picha uchwara lakini serikali inawatambua na kuwaendeleza na hatimaye wanakuwa matajiri wa kutupwa...

We unavyodhani hii ni sura ya nani...

1 comment:

Anonymous said...

abdujumbe uyo!

Website counter